Akizungumza na Kipindi cha Dakika 45 kilichorushwa hewani Jumatatu usiku na Runinga ya ITV, Nyerere alisema baada ya uchunguzi kufanyika ilibainika kuwa yale madawa kwa nchini Afrika Kusini si ya kulevya lakini kwa Tanzania ni ya kulevya.
Alisema kutokana na kubainika kwamba yalitokea nchini, baadhi ya wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar walitimuliwa kazi, akasema basi ilikuwa lazima Masogange baada ya kutua Bongo akamatwe.
“Mimi nimeshangaa sana jamani, ilikuwaje watu watimuliwe kazini pale uwanja wa ndege kwa kuwatuhumu kuruhusu madawa ya kulevya kupita, kwa nini walimuachia huru yule binti (Masogange), basi waliofukuzwa nao warudishwe kazini,” alisema Nyerere.
Paparazi wetu, juzi alifanya jitihada za kuzungumza na Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Harrison Mwakyembe lakini simu yake ilikuwa ikiita tu.
Kwa upande wake, Kamanda wa Kikosi Maalum cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Afande Godfrey Nzowa alipopigiwa simu alisema kule Afrika Kusini Masogange alipatikana na hatia na kuhumumiwa, kwa hiyo hakuna sheria ya kumkamata tena hapa nchini.
“Kule alihukumiwa kwenda jela au kulipa faini, ina maana alipatikana na hatia, akalipa faini na kuachiwa, sasa kwa nini tumkamate huku?” alihoji Nzowa.
Simu ya Masogenge juzi ilikuwa ikiita mara kadhaa bila kupokelewa.
Julai 5, mwaka jana, Masogange na Melisa Edward walikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg na madawa ya kulevya aina ya crystal methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.

