Sports


BIFU: WILSHERE AMTIMUA KINDA LA MAN UTD ENGLAND

Kiungo wa England, Jack Wilshere

KAULI iliyotolewa na kiungo wa Arsenal na timu ya taifa ya England, Jack Wilshere ni sawa na kumtimua kinda wa Manchester United, Adnan Januzaj ambaye amekuwa akipigiwa debe kuichezea England.

Wilshere alipoulizwa juu ya sakala hilo alijibu, ‘Waingereza pekee ndiyo wanatakiwa kuichezea timu ya taifa ya England’.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 18, alimesajiliwa na Manchester United msimu huu anaweza kuichezea England kama akipata kibari kutoka Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) baada ya kuishi nchini humo kwa miaka mitano.

Kiungo huyo ambaye wiki iliyoipita aliisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sunderland kwa kufunga mabao yote mawili ana uhuru wa kuchagua timu moja ya taifa ya kuichezea kati ya Ubelgiji, Serbia, Albania na Uturuki.

Kinda la Manchester United, Adnan Januzaj akishangilia moja ya mabao yake akiwa na wachezaji wenzake

Wilshere alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema: "Kama umeishi England kwa miaka mitano haimaanishi kuwa wewe ni Mwingereza."

“Tuna wachezaji wengi sana katika kikosi cha timu yetu ambao hawajazaliwa hapa na familia zao pia hazipo hapa nchini lakini hawazichezei hizo nchi walikokuwa wazazi wao.”