Sunday 16 February 2014

HIVI NDIVYO NGASA ALIVYO MZAWADIA DIAMOND MAGOLI YAKE..CHEKI WALIVYO KUTANA NDANI YA NDEGE


  Mrisho Khalfan Ngassa jana alifunga tena mabao matatu peke yake katika ushindi wa 5-2 wa Yanga dhidi ya wenyeji Komorozine ya Comoro katika mchezo wa marudiano, Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika. Ngassa ambaye pia alifunga hat trick wakati Yanga inaichapa mabao 7-0 Komorozine katika mchezo wa kwanza Dar es
Salaam, ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba mabao yake yote hayo amzawadia mwanamuziki rafiki yake kipenzi, Diamond pichani kulia, kwa sababu alimtabiri atafunga idadi hiyo ya mabao kabla ya mechi hiyo. Ngassa na Diamond ni marafiki walioshibana na wamewahi kufanya tangazo la biashara pamoja

source-binzuberi