Sunday 16 February 2014

ANGALIA PICHA AJALI ZA MAGARI ZINAVYOKATISHA MAISHA YA BINADAMU

Watu watatu akiwemo dereva wa gari ndogo aina ya Ford fiesta nyeusi na wanawake wawili wamepoteza maisha katika ajali mbaya iliyohusisha  gari aina ya Ford fiesta nyeusi na lori aina ya mercedes 1318.Tukio hili ambalo limetokea katika mji wa Crateus jimbo la kaskazini mashariki nchini Brazili liliripotiwa kuwa ndani ya gari hiyo ya Ford fiesta kulikuwemo na watu watano wanaume watatu na wanawake wawili.Lori hilo ambalo liligonga  gari dogo kwa upande wa kushoto lilisababisha dereva na wanawake wawili walio kuwa wamekaa siti ya nyuma ya gari hilo kupoteza maisha papo hapo mda mchache baada ya ajali hiyo kutokea.
Katika ajali hiyo vijana wengine wawili kati ya hao watano walijeruhiwa vibaya huku wale waliokuwa katika lori wakitoka salama bila kupatwa na majeraha ya aina yeyote.