Habari
zilizotufikia katika chumba chetu cha habari kwamba basi la kampuni ya
Japanese Express linalofanya safari zake kati ya Makete - Njombe,
limetumbukia kwenye mto eneo la Lwamadovela wilayani Makete
Basi
hilo lilikuwa likitokea Njombe kuja Makete na ajali hiyo imetokea
majira ya saa 11 jana jioni kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo
Taarifa kamili ya ajali hiyo pamoja na picha zitakujia baada ya kikosi kazi cha Eddy Blog kufika eneo hilo
