Habari za
kuaminika zilizopatikana kutoka vyanzo mbalimbali ndani ya CCM, zinasema
Baraza la Ushauri, linaloundwa na marais wastaafu, linatarajia kutoa
tamko zito kutokana na mwenendo unaoonyeshwa na makada wake.
Baraza hilo, linaundwa na wenyeviti na makamu wastaafu wa chama, likiongozwa na Mwenyekiti wake, Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Katibu wake ni Pius Msekwa.
Wengine ni Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Amani Abeid Karume na Waziri Mkuu mstaafu, John Malicela.
Hatua hiyo
imekuja siku chache baada ya kuibuka malumbano yanayowahusisha makada wa
chama hicho wanaotajwa kuwania mbio za urais mwaka 2015 kuanza harakati
mapema.
Kwa mujibu
wa chanzo cha kuaminika kutoka CCM, kiliiambia MTANZANIA kuwa kikao cha
CC, pamoja na mengine, kitatoa dira ya chama na kuweka mikakati ya
kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
"CC itakutana Februari 9, mwaka huu kati ya mjini Dodoma au Dar es Salaam, lakini katika kikao hicho wajumbe wa Baraza la Ushauri la chama watakuwepo.
"Sijui
watazungumza nini katika kikao hicho, huenda ikawa haya mambo
yanayoendelea ndani ya chama hivi sasa, kwani tambua wajumbe wa baraza
wanaweza kuomba kukutana na CC au NEC wakati wowote pale wanapoona
inafaa," kilisema chanzo hicho.
Katika siku za hivi karibuni, makada wa CCM wameibuka na kuunga mkono hatua ya Katibu wa Uhamasishaji wa Chipukizi, Paul Makonda, ambaye alimtuhumu Waziri Mkuu wa zamani, EdwardLowassa, kuwa ameanza harakati za kuwania urais.
Baada ya kauli hiyo, Malecela naye aliibuka na kuutaka uongozi wa CCM kumchukulia hatua Lowassa.
Malecela alidai, Lowassa anakiyumbisha chama hicho kutokana na kampeni za kutaka kuwania urais wa 2015.
Alisema
Sekretarieti ya CCM inapaswa kuwachukulia hatua kali makada
wanaojipitisha maeneo mbalimbali nchini kwa nia ya kusaka urais, kabla
ya cha