kutumia usafiri wa bodaboda.
Josephine Michael akiwa barabarani baada ya kujifungua.
Tukio hilo lililowashtua watu wengi
lilitokea asubuhi kwenye Kituo cha Daladala Cha Nanenane kandokando ya
Barabara Kuu iendayo Dar es Salaam.
Mwandishi wetu alifika eneo la tukio
na kumshuhudia askari wa kike wa kikosi cha usalama barabarani ‘trafiki’
(jina lake halikupatikana) akiacha kazi ya kuongoza magari na kugeuka
mkunga kwa muda ili kumsaidia binti huyo akiwa sambamba na wanawake
wengine na kufanikisha kupatikana kwa mtoto wa kiume ‘dume la nguvu’.
Mmoja wa akina mama waliofika eneo hilo akiwa amembeba mtoto wakati mama yake akihojiwa na mwanahabari.
Awali, wanawake hao walizungusha kanga ili kuweza kuweka usiri wakati wa kumsaidia mwanamke mwenzao alipokuwa akijifungua.
Mara baada ya zoezi hilo kwenda
salama, Josephine alisema alipatwa na uchungu alfajiri ya siku hiyo na
mume wake aliwapigia simu madereva wa teksi zaidi ya wawili ambao
waligoma kufika kijijini kwao kutokana na ubovu wa barabara.
Kulia ni trafiki aliyemsaidi Josephine kujifungua na kushoto mtoto aliyezaliwa akiwa amebebwa.
“Hali
ilipozidi kuwa mbaya tuliwasiliana na dereva wa bodaboda ambaye alifika
na kunibeba huku mume wangu akitufuatilia nyuma kwa baiskeli yake,”
alisema Josephine kwa uchangamfu.
Binti huyo alisema kwamba walipofika
eneo la Nanenane hali ilizidi kuwa mbaya akashindwa kujizuia baada ya
mtoto kushuka chini, hivyo akamuomba dereva wa bodaboda asimame ndipo
alipoanguka chini na hali kuzidi kuwa mbaya.
Wananchi waliofika eneo hilo wakiwa na Josephine (aliyekaa chini).
Baada ya kuliona tukio hilo, trafiki na wanawake wengine waliokuwa jirani wakajitolea kumsaidia hadi alipojifungua salama.
Dereva wa bodaboda aliyembeba
Josephine anayejulikana kwa jina la Gitogo Shilagi alikiri barabara
iendayo Kijiji cha Kiegea kuwa mbovu.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa baada ya Josephine kujifungua salama mtoto wa kiume