Mambo vipi ? samahani lakini inabidi niwe wa kwanza
kukwambia haya, ni vema wangekwambia rafiki zako wa karibu lakini
kwasababu hawajaweza kukwambia basi hainabudi nikwambie mimi.Kuna tabia
fulani zinazokufanya usifikie malengo ambayo unayafikiriaga muda
wote.Sikulaumu, sisi wote hua mara moja au nyingine tunaangukia katika
mambo haya.Sasa ni wakati wa mabadiliko kwasababu hivi ndio vitu
vinavyozuia mafanikio yako.
Unatumia muda mwingi Facebook
Najua si vibaya kucheki what friends are up to now and then lakini
muda unaotumia kulike status na picha za watu ambazo hazileti tofauti
yoyote katika maisha yako unasababisha upoteaji wa muda mwingi .
Ni kweli unatumia siku nzima ofisini lakini mapumziko ,kusumbuliwa na
kupoteza kusudi la kazi unayofanya vinachangia sana kupoteza muda wako
kwa kiasi usichoweza kutegemea.Ushawahi kufikiria biashara ya pembeni
itakayokuletea kipato ? je , unafanya nini muda wa kazi unapoisha? Je,
unatumia muda wako wa jioni kukaa kwenye kochi ukiangalia TV au laprop
ukicheki movies/series ? Huo ndio muda ambao unatakiwa ufikirie business
idea uliyonayo, kazi ya nje au kitu chako mwenyewe ambacho kwa siku za
baadae kitakua ndio kazi yako ya kudumu.
Hauna Ufanisi
Kwahiyo unaweza kusema unafanya kazi kwa bidii na haupotezi muda wako
katika kazi zako lakini nataka nikuambie na sipendi kusema hivi –
unaweza kufanya vizuri zaidi. Bdio, unafanya kazi kwa bidii lakini kuna
njia ya kufanya kazi hiyo izae matunda.unajua msemo unaosema” Siyo tu
ufanye kazi kwa bidii, bali ufanye kazi nadhifu.”
Unakata tamaa kirahisia
labda mambo hayajaenda kama ulivyotarajia au watu
hawadhamini mchango wako na hii kukufanya kukosa motisha na msukumo wa
kufanya kazi. Hauwezi kufikiria malipo ya miaka ijayo kwa kazi
unayoifanya leo kazi utazofanya kwa siku,wiki hata mwezi na kulipwa ni
nzuri na ndio ambazo watu wengi hupendelea.lakini kwa kila mtu
aliyefanikiwa anajua kwamba ili uweze kujenga kitu au biashara imara na
endelevu inabidi uwekeze katika muda sasa na matokeo yake
hayatajionyesha kwa miaka.kama hauwezi kukubaliana na jambo hili basi
utakua haufikirii kwa upeo zaidi mambo ya baadae.
Hau-take Risks
Najua.Ni vizuri zaidi kutoamua kutofanya kitu ambacho kinaweza
kukwama baadae. kuacha ku-take risks ni vizuri lakini hakuna malipo bila
kufanya kitu cha hatari kidogo. najua kuna vitu vizuri vinaweza kutokea
bila mtu ku-take risk lakini ni mara ngapi biashara inajegwa na kukua
kwa kutegemea bahati halisi.Taking risks inabidi iwe moja ya job
description yako na japokua ukifeli haujisikii vizuri lakini unajua kipi
kitakufanya ujisikie vizuru? kufeli , kufeli , kufeli na ghafla kufaulu
na kufanikiwa. na sasa hautajisikia vibaya kuhusu kufeli kwako sababu
kupitia kufeli huko ndio kulikufunza njia ya kufaulu.
Hautumii Opportunities
sio tu kuchukua risks bali hata kuchukua opportunities zinazotokea
linaweza likawa jambo gumu. opportunities zenyewe zinakuja kwa kujificha
ukitofautisha na risks.maranyingi mafanikio huja kwa kukubali kuchukua
opportunities zinazotisha. tafuta opportunities kwenye sehemu
ulizotegemea na utashangaa vitu utakavyogundua.
Naamini unaweza kufanikiwa,inabidi tu kuangalia hivi vitu 7 nilivyovizungumzia.