Tuesday, 1 July 2014

ANGALIA PICHA SAFARI YA MWISHO YA MWANAFUNZI DANIEL LEMA ALIYECHOMWA MOTO KWA KUTUMIWA KUWA MWIZI


Mwili wa Daniel Lema ukiagwa na baadhi ya wanachuo pamoja na raia waliojitokeza kuhudhuria ibada ya kuuaga mwili wa marehemu mapema asubuhi ya leo katika hospitali ya rufaa mkoani iringa.

Mwanafunzi (LEMA) aliyejeruhiwa kwa moto

  Baadhi ya raia walijitokeza kumuaga Lema katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa mkoani Iringa.











LEMA Aliyekua akisoma mwaka wa 4 kozi ya sheria katika chuo kikuu kishiriki cha Mt.Augustino Tawi la Iringa (Ruaha University College-RUCO), mwanzoni mwa wiki hii ameshambuliwa kwa kuunguzwa na moto akidhaniwa ni mwizi.
Mnamo tarehe 24.06.2014 mwanafunzi huyo alikua ametoka kuangalia michuano ya kombe la dunia na akiwa amelewa akawa anatafuta chakula cha jioni na ilikua majira ya saa 5 Usiku, Mwanafunzi huyo aliingia kwenye mgahawa ambao biashara ilikua imefungwa kwa muda huo lakini ndani kulikuwapo na binti ambaye alianza kupiga kelele kwa kudhani alikua mwizi.
Na kwakua eneo hilo kulikuwa na mlinzi(Mmasai) ndiye aliyeanza kumshambulia mwanafunzi huyo.
Baada ya tukio hilo wakatokea watu  (2) waliojitambulisha kuwa ni askari wakaamuru mwanafunzi huyo asipigwe kwa madai ya kumfikisha kituoni.
Lakini baada ya mwendo mfupi kuelekea kituoni mwananchi mmoja alimchukua kijana huyo kinguvu kisha kumwagia mafuta na kisha kumuwasha moto, ambao ulizimwa na madereva bodabora walio kuwa eneo hilo na kisha kumkumbiza kijana huyo hospitali.
Mpaka sasa Kijana huyo amelazwa katika wodi ya watu mahututi (ICU) katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa ambapo mama yake mzazi pamoja na kaka yake ndio wanaomsaidia kumuhudumia.
Mwili wake umeagwa mapema leo katika hospitali ya rufaa mkoani Iringa tayari kwa safari ya kuelekea mkoani Kilimanjaro kwaajili ya mazishi yatakayofanyika siku ya juma tano.
Lema alizaliwa mnamo tarehe 05/06/1989 na kufariki tarehe 30/06/2014 Mungu na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi!!!