June
20 2014 Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ni miongoni mwa waliowasha
vipaza sauti kwenye
bunge la bajeti linaloendelea Dodoma (104.4 Clouds
FM) ambapo sehemu ya alichochangia ni hiki kinachofata hapa.
‘Dola bilioni moja miaka kumi nyuma ilikua ni Trilioni 11 lakini sasa
unaongelea Trilioni 17 kwa hiyo shilingi imeshuka thamani lakini
unashangaa kwanini tunaendelea kuongeza ushuru kwenye pombe na sigara
kama chanzo cha mapato ya taifa letu, nchi nyingi duniani zinazoongeza
ushuru kwenye pombe na sigara lengo lake ni kuona idadi ya wanaokunywa
na kuvuta inapungua tofauti na Tanzania ambako lengo limekua ni
kukusanya mapato, hiki ni kitu cha kusikitisha sana’
‘Nimekwenda Singida hivi karibuni kwenye ziara ya chama chetu na Mh.
Tundu Lissu, ukiwa Singida na Dodoma unaona kuna jua kali… Singida Same
serikali imeweka vibao barabarani >> NENDA POLEPOLE HAPA KUNA
UPEPO MKALI UNAUA << ingekua ni taifa kama Israel, upepo mkali
hauwekewi vibao vya kuua bali upepo mkali unachukuliwa kuwa umeme’
‘Sehemu kubwa ya Singida na Dodoma ni semi desert, serikali ingeweza
kabisa kutengeneza solar village maeneo haya ikatengeneza umeme mkubwa
kupitia nguvu za jua ukaingizwa kwenye gridi ya taifa na mngeweza
kupunguza bili za umeme ambazo Wananchi kwa sasa wanapigwa huko mitaani’
‘Hata
kama kutakua na mpango wa aina gani, unapokua na serikali ambayo
haifikirii kwa upana… serikali ambayo inasema bado inakopesheka, bado
tunaweza kukopesheka…. mimi ningekua ni nyinyi, ningekwenda kukopa
barabara zote nchi nzima zijengwe, ningeenda kukopa reli ijengwe,
ningekwenda kukopa Airport ziboreshwe na ningekwenda kukopa serikali
yenu ihamie hapa Dodoma’
‘Watu wengi wamesema kuhusu serikali kuhamia hapa Dodoma, ukiondoa
serikali Dar es salaam ukaileta Dodoma utaipa nguvu hii Ruaha ambayo
hakuna watalii, watalii wataanza kwenda kwa sababu watu watakuwa
wanakuja Dodoma kufanya mikakati yao kwa hiyo centre ya mapumziko itakua
ni Iringa, Mbeya na Singida’
‘Mimi ningekua nyinyi ningefanya maamuzi magumu, ningechukua Mawaziri
wote na makatibu wakuu wote waje hapa wakae gesti na wengine wakae
kwenye matent kwa sababu msipochukua maamuzi serious hamuwezi kuibadili
hii nchi, hii nchi haitobadilishwa kwa Kinana kuzunguka kutafuta kura za
Urais huko kote anakokwenda’
Unampa asilimia ngapi Mbunge huyu kwa alichoongea? acha maoni yako kwenye comment hapa chini