MSHAMBULIAJI
Wayne Rooney hatakiwi kubeba lawama kwa England kutolewa mapema katika
Kombe la Dunia, amesema Robin van Persie, ambaye ameishauri FA ya nchi
hiyo kutazama msingi wake wa soka ya vijana.
Van
Persie amesema Rooney na England walicheza vizuri dhidi ya Uruguay
kiasi cha kutosha kushinda na kusonga mbele, na akamfagilia mshambuliaji
mwenzake wa Mancheser United, ambaye alishutumiwa vikali baada ya
kipigo cha England katika mechi ya kwanza dhidi ya Italia.
"Niliangalia
sehemu kubwa ya mchezo dhidi ya Italia na mchezo wote dhidi ya Uruguay,
na ninafikiri ni aibu. England ilicheza vizuri mno na hawakuwa na
bahati kabisa. Wayne alipambana sana, alicheza vizuri sana na angeweza
kufunga mabao manne, hivyo sifikiri ni wa kulaumiwa.
Wayne Rooney alipambana sana dhidi ya Uruguay
"Wayne
ni mchezaji mkubwa. Nimesema hive mara nyingi, Wayne alikuwa sehemu ya
sababu mimi kuja Manchester United. Sijawahi kujuta kusema hivyo, kwa
sababu kwa kufanya nays mazoezi na kucheza nays ananioyesha ni mchezaji
wa kiwango cha dunia.
"Alipiga
mpira wa adhabu vizuri mno, alipiga shuti zuri lililookolewa na kipa,
alipiga kichwa kilichogonga mamba wa juu na akafunga bao. Si wa kulaumu,
Alijitoa kwa kitu kwa ajili ya nchi yake. Ni haki kumshutumu sana yeye.
"Alipoteza
nafasi tatu za kufunga kwa inchi chache, na hiyo maana yake alikuwa
katikati ya mstari wa kushinda na kushindwa, baina ya kurudi nyumbani na
kusonga mbele.’
Wawili hatari: Wayne Rooney (kushoto) na Robin Van Persie (katikati) wakiwa mazoezini Man United
Na
Van Persie anaamini FA inapaswa kutazama muundo wake makocha na
kuwekeza zaidi katika maendeleo ya vijana, kama ilivyo kwa Uholanzi na
nchi nyingine zinazoongoza Ulaya: "Sasa ni juu ya FA kuwa na mtazamo
sahihi ili kuona England itaelekea wapi.
"Ni muhimu sana kuwekeza kwenye soka yaw vijana, katika makocha wazuri na vifaa kwa ajili ya nyota chipukizi kucheza,"amesema.