Baadhi ya wagonjwa wakiwa wametolewa hospitali ya TMJ baada ya nyumba ya jirani kuwaka moto. Walitolewa wodini kwa tahadhari.
Kikosi
cha Kuzima Moto kikizima moto nyumba jirani na Hospital ya TMJ iliyopo
Mikocheni Dar es Salaam muda huu na watu kudhani kuwa iliyokuwa ikiungua
ni hospitali.Tahadhari hiyo ilichukuliwa kutokana na wasiwasi kuwa moto huo ungeweza kuvuka na kuingia hospitali lakini ulidhibitiwa na kikosi cha zima moto na kuishia katika nyumba hiyo ya jirani.
