MANCHESTER
City imerudi kwa hasira katika Ligi Kuu ya England ikitoka kutolewa
Ligi ya Mabingwa Ulaya- baada ya jioni hii kuifumua mabao 5-0 Fulham
katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester.
Mwanasoka
Bora wa Afrika, Yaya Toure leo amepiga hat trick yake ya kwanza, mabao
mawili akifunga kwa penalti dakika ya 26 na 54 na linguine dakika ya 65
akimalizia pasi ya Samir Nasri.
Mabao
mengine ya Man City yamefungwa na Fernandinho dakika ya 84, akimalizia
pasi ya Milner na Demichelis dakika ya 88. Ushindi huo, unaifanya City
ifikishe pointi 63 baada ya kucheza mechi 28 na kupanda nafasi ya tatu
mbele ya Arsenal yenye pointi 62 za mechi 30.
Chelsea
inaongoza Ligi Kuu England kwa pointi zake 69 za mechi 31, ikifuatiwa
na Liverpool yenye pointi 65 baada ya mechi 30, wakati Arsenal yenye
pointi 62 ni ya nne.
