MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Uruguay, Luis Suarez amepiga hat trick timu yake,
Liverpool ikiifunga mabao 6-3 Cardiff City katika mchezo wa Ligi Kuu ya
England jioni Uwanja wa Cardiff.
Cardiff
walitangulia kupata bao dakika ya tisa mfungaji Mutch kwa pasi ya
Campbell, lakini Luis Suarez akaisawazishia Liverpool dakika ya 16 kwa
pasi ya Johnson.
Campbell
aliifungia bao la pili Cardiff dakika ya 25 pasi ya Mutch na Martin
Skrtel akaifungia Liverpool mara mbili mfululizo dakika ya 41 na 54,
mabao yote pasi za Philippe Coutinho kabla ya Suarez kufunga la nne
dakika ya 60 akimalizia pasi ya Daniel Sturridge.
Sturridge
alifunga bao la tano dakika ya 75 kwa pasi ya Suarez kabla ya Mutch
kuifungia Cardiff la tatu dakika ya 88, pasi ya Jones. Suarez
alikamilisha hat trick yake dakika ya sita ya muda wa nyongeza baada ya
kutimu dakika 90 za kawaida kwa bao la sita akimalizaia pasi ya Skrtel.
