TOUT
Puisant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) tayari wapo
Abidjan, Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Hatua ya 16 Bora
Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Sewe Sport jioni ya kesho.
Timu
hiyo yenye washambuliaji wawili wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na
Thomas Emmanuel Ulimwengu imekuwa na habati kuanzia ugenini hatua hiyo,
kama itapata matokeo mazuri ya awali, itafurahia kucheza mechi ya
marudiano mbele ya mashabiki wake wenye sapoti kubwa mjini Lubumbashi.
Mabingwa
watetezi, Al Ahly ya Misri walioitoa Yanga SC kwa penalti 4-3 kufuatia
sare ya jumla ya 1-1, wao pia wataanzia ugenini kesho dhidi ya Ahly
Benghazi ya Libya.
Horoya
ya Guinea itaanzia nyumbani na CS Sfaxien ya Tunisia, sawa na ES Setif
ya Algeria itakayoikaribisha Coton Sport ya Cameroon, AC Leopards ya
Kongo itakayoikaribisha Al-Hilal ya Sudan na Nkana ya Zambia
itakayoikaribisha Zamalek ya Misri.
Timu
nyingine ya DRC, AS Vita itaanzia nyumbani na Kaizer Chiefs ya Afrika
Kusini Uwanja wa Tata Raphael mjini Kinshasa, wakati mechi zote za
marudiano zitachezwa Jumamosi ya Machi 29, mwaka huu
