WAKALA
wa kinda wa Manchester United, Marnick Vermijl amesema kwamba mteja
wake atapenda kubakia Old Trafford iwapo tu kocha David Moyes ataondoka.
Beki
wa pembeni Mbelgiji, Marnick Vermijl mwenye umri wa miaka 22, amechezea
mara kadhaa kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 21 cha timu yake
ya taifa na kwa sasa yupo kwa mkopo NEC Nijmegen msimu huu.
Akizungumza na Hets Nieuwsblad,
wakala wa Vermijl aitwaye Tony Dullers amesema: "Yupo ndani ya mkataba
na Manchester United hadi Juni 2015, lakini zaidi itategemea na
mazingira ya David Moyes.
Zao la uzalishaji vijana: Mbelgiji huyo alitua Manchester United akitokea Standard Liege mwaka 2010
"Kwa
Manchester United, wanafurahia sana maendeleo yake. Wanataka Marnick
afanye kazi katika klabu bora msimu ujao, lakini si kutolewa kwa mkopo
tena. Aidha anaweza kupata nafasi katika kikosi cha kwanza, au kuuzwa
moja kwa moja,".
Dullers
amesema kwamba Ajax na klabu nyingine kadhaa za Ligi Kuu Engand
zimeonyesha nia ya kumsajili beki huyo, wakati atakutana pia na Genk na
Anderlecht wiki zijazo.
Majukumu ya kimataifa: Mchezaji huyo wa Man United ameichezea mechi kadhaa U21 ya Ubelgiji
