Hii
ni ajali iliyotokea mchana wa March 21 nje ya gheti la kutokea kituo
cha mabasi yaendayo mikoani[Ubungo Bus Terminal]na imehusisha lori
lililofeli breki na kwenda kugonga magari 5,mpaka sasa idadi kamili ya
majeruhi na watu waliopoteza maisha haijapatikana.Jeshi la Polisi tayari wameshaanza kuchukua hatua za awali ikiwa ni pamoja na kuwapeleka majeruhi hospitali na kutoa magari yaliyosababisha ajali hiyo,kwa taarifa za awali inasemekana Dereva wa lori hilo alikimbia mara baada ya kutokea ajali hiyo,


Miongoni mwa majeruhi wa ajali hiyo wakikimbizwa hospital.





