Kufuatia kipigo walichokipata wiki
iliyopita kutoka kwa Aston Villa cha bao 1-0, Kocha mkuu wa klabu ya chelsea
merno Jose Mourinho amejikuta yuko hatiani baada ya kile kinachodaiwa ni utovu
wa nidhamu.
Katika pambano hilo Mourinho
alijikuta anatolewa nje ya uwanja,kwa kitendo chake cha kuingia ndani ya
uwanja kuongea na mwamuzi Chris Foy baada ya kiungo wake wa kibrazil Ramires
kuonyeshwa kadi nyekundu dakika za lala za salama.
Mourinho ameamriwa
mpaka Jumatatu awe amejibu tuhuma kwa Chama cha Soka England.Mreno huyo, ambaye
pointi za uongozi katika ligi zilipunguzwa kufuatia kipigo hicho, alimlaumu
mwamuzi Foy baada ya mchezo katika uwanja wa Villa Park.
