KOCHA
Manuel Pellegrini anaamini Manchester City wanaweza kushinda michezo
yote 11 zilizobaki na kubeba taji la Ligi Kuu ya England - lakini
watalazimika kucheza bila mfungaji wao bora Sergio Aguero katika mechi
zisizopungua mbili.
Mshambuliaji
huyo wa Argentina, ambaye alfunga bao lililoipa ubingwa City katika
mechi ya mwisho msimu wa 2012, atakuwa nje kuanzia mechi ya leo dhidi ya
Fulham na Jumanne dhidi ya wapinzani, Manchester United kutokana na
maumivu ya ya nyama za paja.
Pellegrini anatarajia Aguero kufanya mazoezi wiki ijayo,lakini pia anaweza kukosa pia mechi dhidi Arsenal wikiendi ijayo.
Alipoumia: Aguero alipata maumivu wakati City ikitolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na Barcelona
"Sina uhakika kuhusu Arsenal," alisema kocha huyo City. "Tutaona atakaporejea, lakini hana nafasi kabisa katika mechi United. "Labda wiki ijayo ataanza kufanya kazi na wenzake,lakini sifikiri kwa wiki yote,".
City
inaachwa na vinara Chelsea kwa pointi sita, lakini bado wana nafasi ya
ubingwa kutokana na kuwa na mechi tatu mkononi, na Pellegrini anaamini
wachezaji wake wanaweza kuendeleza wimbi la ushindi hadi mwisho wa
msimu.
