KOCHA
Arsene Wenger amemtuhumu Arjen Robben kujirusha na kumponza kipa wa
Arsenal, Wojciech Szczesny kutolewa nje kwa kadi nyekundu, ambayo
ilisababisha wafungwe mabao 2-0 na Bayern Munich.
Mwalimu
huyo Mkuu wa Arsenal pamoja na kulalamikia kitendo hicho, pia alisema
wachezaji wengine wa Bayern walimtumia vibaya refa Nicola Rizzoli.
"Kipa alimgusa kweli, lakini nilimuambia Robben aliongeza chumvi na ilibadilisha mchezo.
"Siyo
tu ilibadilisha mchezo, iliua mchezo. Ulikuwa mchezo wa ubora wa hali
ya juu na katika kipindi cha pili ulikuwa unaelekea mwisho," alisema
Wenger.
Macho kwenye mpira: Robben akipokea mpira wa juu katika eneo la hatari la The Gunners huku Szczesny akipiga hesabu za kuokoa
Faulo? Inaonekana kama Szczesny anamkwatua mguuni Robben
Wawili hao walienda chini wote na refa Nicola Rizzoli akatoa penalti na kadi nyekundu
Robben akiugulia maumivu huku Szczesny akimuangalia
Robben
alianguka chini wakati akigombea mpira ma kipa huyo wa kimataifa wa
Poland, ambaye alipewa kadi nyekundu ya moja kwa moja.
Wenger
alimnyooshea mikono Robben kumshutumu kwamba alijiangusha kutafuta
penalti. David Alaba akakosa penalti hiyo, lakini wachezaji 10 wa
Arsenal hawekuweza kuwazuia Toni Kroos na Thomas Muller kuifungia Bayern
katika ushindi wa 2-0.
Mesut Ozil pia alikosa penalti upande wa The Gunners na kuna hatari Szczesny akaadhibiwa zaidi na UEFA kwa kuonyesha ishara mbaya jukwaani baada ya kutolewa.
Refa wa Italia akimuonyesha kadi nyekundu Szczesny iliyoimaliza Arsenal
