INAKADIRIWA
kiasi cha watu milioni 1.6 watapatwa na ugonjwa wa saratani mwaka
nchini Marekani na inakadiriwa kuwa kati ya hao, watu laki 5 watapoteza
maisha kutokana na
ugonjwa huo hatari. Pia kiasi cha watu laki 6
hufariki kwa ugonjwa wa moyo nchini humo kila mwaka.Licha
ya maendeleo ya kisayansi yaliyopatikana kwa nusu karne iliyopita,
lakini makampuni ya kimagharibi yanayotengeneza dawa za binadamu,
yameshindwa kuvumbua dawa madhubuti ya kudhibiti magonjwa haya mawili
yanayouwa watu wengi zaidi duniani.
Inaelezwa
na watafiti wa masuala ya afya nchini Marekani kuwa hivi sasa
imedhihirika kuwa mikakati mingi ya kisasa, kuanzia kwenye vipimo hadi
matibabu ya magonjwa ya moyo na saratani, imeshindwa kufanya vipimo na
kutoa matibabu sahihi, wakati mwingine kwa kukosea, tiba ya magonjwa
haya huwa na madhara zaidi kwa mgonjwa kuliko ahueni.
Soda na hatari ya saratani
Kwa
mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, wanawake wenye umri kuanzia miaka
40, ambao hunywa kwa wingi soda au vinywaji vingine baridi vyenye sukari
nyingi, wako katika hatari kubwa ya kupatwa na saratani ya kizazi.
Imeelezwa
kuwa utafiti huo ni wa uhakika kwa sababu matokeo hayo yamepatikana
baada ya kuwafanyia utafiti wanawake waliofikia ukomo wa hedhi
(postmenopausal) wapatao 23,000 kwa kuwafuatilia kwa muda wa miaka 14.
Katika
utafiti huo, ilibainika kuwa wanawake waliokuwa na matumizi makubwa ya
sukari walikuwa katika hatari kubwa ya kupatwa na saratani ya kizazi kwa
asilimia 78. Kwa mujibu wa mwandishi wa utafiti huo, Bw. Maki
Inoue-Choi, hakushangazwa na matokeo ya utafiti huo kwani imekuwa
ikisemwa kwa muda mrefu kuwa sukari nyingi ina madhara.
Aidha,
utafiti mwingine unaonesha kuwa ‘fructose’ (aina ya sukari) huimarisha
ukuaji wa chembechembe hai za saratani na kuharibu mifumo kadhaa mwilini
kwa njia mbalimbali, ikiwemo kuharibu mfumo wa usagaji chakula tumboni,
ukuaji wa seli za DNA na kinga ya mwili.
Baada
ya utafiti huo, wagonjwa wa saratani za aina zote hushauriwa kutotumia
kabisa vyakula vyoyote vyenye sukari, kwani kwa kufanya hivyo huwa
wanauimarisha zaidi ugonjwa badala ya kuudhibiti. Sukari ni miongoni mwa
vyakula vinavyoimarisha chembechembe hai za saratani, hivyo kuvinyima
sukari ni njia moja wapo ya kuviua na kuvipa sukari ni sawa na kuvifuga.
Pamoja
na utafiti huo kuonesha kuwa chakula cha seli za saratani ni
‘fructose’, haikukatazwa watu kula matunda ambayo huwa na ‘fructose’,
badala yake wameshauriwa kupendelea kula matunda zaidi kuliko juisi
yake. Kimsingi ‘fuctose’ asilia iliyomo kwenye matunda haiwezi kuwa na
madhara kwa mwili wa binadamu kama ilivyo kwa ‘fructose’ za kutengeza
zinazotumika zaidi kwenye vyakula na vinywaji mbalimbali baridi.
Mwisho,
pamoja na kuwa kwamba sukari ni bidhaa muhimu kwa matumizi ya binadamu
ya kila kila siku na kwamba sukari pia ina faida mwilini, lakini ni
vyema ikaeleweka siyo bidhaa salama unayoweza kuitumia utakavyo. Pale
ambapo hatuna budi, basi tuitumie kwa uchache sana na pale ambapo
tunaweza kuiacha kuitumia kabisa, bora tukafanya hivyo.