ITV, EATV, Channel Ten, Star TV na vituo vingine vya runinga Tanzania
vimepata mpinzani mwenye nguvu. Ni kituo kipya kiitwacho TV1. Kituo
hicho kinamilikiwa na kampuni ya Sweden iitwayo, Modern Times Group.
Kampuni hiyo iliyojikita zaidi kwenye masuala ya burudani imeanzisha
kituo hicho mapema mwaka huu na kwake ikiwa ni TV ya kwanza ya bure
kuwahi kuianzisha.
TV1 itakuwa ni channel ya burudani itakayokuwa pia mchanganyiko wa
habari zilizoandaliwa nyumbani na za kimataifa pamoja kurusha filamu za
kimataifa na TV series.
Tayari kituo hicho kimeajiri watangazaji mbalimbali wazoefu kufanya
vipindi mbalimbali wakiwemo Marygoreth Richard aliyekuwa msomaji wa
habari za East Africa Radio, Angel Karashani (TPF6) na aliyewahi kuwa
mtangazaji wa Channel Ten, Nzowa
Newsroom ya TV1 iliyopo Mikocheni, Dar es Salaam. Channel hiyo
tayari inaonekana kupitia ving’amuzi vya Startimes na inawafikia
asilimia 38 ya wananchi wa Tanzania
George Tyson, director wa vipindi wa TV1
Vanessa Mdee akiwa kwenye set ya show yake ‘The One Show’ ya kituo hicho
Vanessa Mdee akifanyiwa make-up
Vanessa Mdee
Watangazaji wa habari wa TV1, Nzowa na Agnes
Angel Karashani.
(Picha kwa hisani ya Bongo5)