Stori iliyoongoza kwa
vichwa vya habari za michezo mwishoni mwa juma lililopita ilikuwa inamuhusu
mshambuliaji Emmanuel Okwi.
Kilichopelea gumzo la mchezaji huyo ilikuwa ni baada ya FIFA kuiandikia barua TFF na kuitaarifu ya kwamba mchakato wa uhamisho wa Okwi toka SC Villa kwenda Yanga ulikuwa hauna tatizo. Lakini pamoja na kutoa taarifa hiyo FIFA bado ilisema yenyewe haina mamlaka ya kumruhusu mchezaji kuichezea klabu yake hiyo mpya zaidi ya kuiagiza TFF kufuatilia wenyewe taratibu za uhamisho wa mchezaji huyo kama zipo sahihi.
Kilichopelea gumzo la mchezaji huyo ilikuwa ni baada ya FIFA kuiandikia barua TFF na kuitaarifu ya kwamba mchakato wa uhamisho wa Okwi toka SC Villa kwenda Yanga ulikuwa hauna tatizo. Lakini pamoja na kutoa taarifa hiyo FIFA bado ilisema yenyewe haina mamlaka ya kumruhusu mchezaji kuichezea klabu yake hiyo mpya zaidi ya kuiagiza TFF kufuatilia wenyewe taratibu za uhamisho wa mchezaji huyo kama zipo sahihi.
Sasa hapo kwenye
kufuatilia taratibu za uhamisho wa mchezaji huyo ndipo kulileta utata,kutokana
na angalizo hilo la FIFA iliulazimu mtandao huu kufuatilia kwa kina kuweza
kujiridhisha na mahusiano yaliyopo hivi sasa kati ya Okwi na klabu ya Etoile Du
Sahel iliyomnunua toka klabu ya Simba.
Baada ya kufanya
mahojiano ya Raisi wa Etoile ndugu Ridha
Charfeddine
aliuhakikishia mtandao huu ya kwamba bado wana mkataba na mchezaji huyo ambao unakwisha
mwezi june mwaka 2016.
Ni vizuri Yanga
wakajiridhisha na haya kabla ya kumchezesha mchezaji husika.
Barua ya Etoile du Sahel waliyomwandikia Okwi wakimsihi arejee klabuni...
USAJILI
FIFA inasisitiza mchezaji kusajiliwa na timu moja tu ya soka kwa wakati mmoja, pia FIFA inasema
wachezaji wanaruhusiwa kusajiliwa na klabu zisizozidi tatu kwa msimu mmoja. Kwa
kipindi hicho mchezaji ataruhusiwa kuchezea timu zisizozidi mbili tu katika
mechi rasmi. Kuna mwiko mmoja tu ambao unaruhusiwa kuvunjwa katika sheria hii, na
huu ni pale ambapo mchezaji atakua amehama kati ya vilabu viwili ambavyo
vinashiriki katika ligi zenye misimu inayofuatana.
Kwa mfano kama mchezaji kahama toka kwenye timu inayoshiriki ligi inayoisha katika mwezi wa tisa kwenda katika timu inayoshiriki ligi inayoanza mwezi wa kwanza, huyu ataruhusiwa kuchezea timu nyingine ya pili katika ligi mpya aliyohamia ili mradi awe ametimiza masharti ya mkataba wake na timu zake zote alizotoka na amezingatia sheria za usajili za chama cha soka cha nchi yake ikiwa ni pamoja na FIFA.
Kwa mfano kama mchezaji kahama toka kwenye timu inayoshiriki ligi inayoisha katika mwezi wa tisa kwenda katika timu inayoshiriki ligi inayoanza mwezi wa kwanza, huyu ataruhusiwa kuchezea timu nyingine ya pili katika ligi mpya aliyohamia ili mradi awe ametimiza masharti ya mkataba wake na timu zake zote alizotoka na amezingatia sheria za usajili za chama cha soka cha nchi yake ikiwa ni pamoja na FIFA.
Maswali ya
kujiuliza
1. Timu ipi kati ya Etoile na Yanga inammiliki mchezaji huyu wakati timu zote
zimemsajili mpaka sasa wakati FIFA wanasisitiza mchezaji kusajiliwa na klabu
moja tu kwa wakati mmoja,
2. kama FIFA wanasema mchezaji
ataruhusiwa kuchezea timu nyingine ya pili katika
ligi mpya aliyohamia ili mradi awe ametimiza masharti ya mkataba wake na timu
zake zote alizotoka. Je Okwi ametimiza masharti na Etoile moja ya timu alizotoka
?
Kuvunja mkataba
Mkataba baina ya mchezaji
wa kulipwa na klabu utaisha pale tu ambapo muda wa mkataba utafikia mwisho wake
au mkataba kuvunjwa kwa makuballiano ya pande zote mbili lakini pia mkataba
unaweza kuvunjwa na pande yoyote ile bila ya kuwa na vipingamizi ama adhabu
pale tu ambapo kutakua na sababu ya muhimu inayotambulika kisheria.
Madhara ya kuvunja mkataba bila sababu maalum.
1. Mara zote upande
unaovunja mkataba ndio unatakiwa kulipa gharama za uvunjaji mkataba.Gharama
zinazohusika kulipwa ni zile zinazohusu mafunzo na kiwango huwa kinahesabiwa
kutokana sheria za nchi,klabu na chama cha nchi husika.Gharama nyingine husika
ni pamoja na madeni ya ada za uhamisho,mshahara wa mchezaji na marupurupu
mengineyo.
2. Jukumu la ulipaji lazima
libebwe na mchezaji ama akishirikiana na timu anayohamia.
3. Ushindwaji wa kulipa
gharama hizi utasababishwa kutolewa kwa adhabu ya kufungiwa kucheza miezi minne
ama miezi sita kutokana na uzito wa kosa. Adhabu hizi zitaanza kutumikiwa mara
baada ya mchezaji husika kupewa taarifa rasmi. Adhabu hizi pia zitasimamishwa
kuanzia mwisho wa msimu hadi mwanzo wa msimu mwingine ndipo zitakapoanza
tena. Ingawa adhabu hizi huruhusiwa kuendelea kama mchezaji husika ni mmojawapo
wa wachezaji katika timu ya taifa inayoshiriki fainali za mashindano
yanayotambulika na FIFA.
4. Kwa ziada ya kulipa
fidia baada ya kuvunja mkataba,adhabu za
ziada zitatolewa kwa klabu ambayo itapatikana na hatia ya kutumia mbinu zisizo
halali za kuchochea uvunjaji wa mkataba kabla ya kipindi kinachoruhusiwa. Klabu
hiyo itafungiwa kusajili mchezaji yoyote kwa kipindi kisichopungua madirisha
mawili ya usajili.
VIPENGELE MAALUM KUHUSU MIKATABA YA WACHEZAJI NA VILABU
Klabu nyingine yoyote yenye nia ya
kuvunja mkataba wa mchezaji na klabu yake ya wakati huo italazimika
kuifahamisha klabu ya mchezaji huyo kwa maandishi kabla ya kuanza mazungumzo na
mchezaji. Mchezaji wa kulipwa ataruhusiwa tu kuanza mazungumzo na klabu nyingine
ikiwa mkataba wake umeisha ama unatarajiwa kuisha ndani ya miezi sita.
Hii ni sehemu ya barua ya FIFA waliyoiandikia TFF... Interview ya Rais wa Etoile
CREDIT SHAFII DAUDA .COM

