Ndege hii ilikuwa imewabeba jamaa na familia za wanajeshi
Redio ya
taifa inasema ndege hiyo aina ya Hercules C-130 ilianguka katika eneo la
milima katika jimbo la Oum El Bouaghi kusini mashariki mwa mji mkuu ,
Algiers na ilikuwa imewabeba abiria 103 wakiwemo wafanyakazi wa ndege.
Miili 71
ya watoto na wanawake imepatikana katika eneo la ajaliKuna taarifa
kwamba ndege hiyo ilikuwa imebeba wanajeshi na jamaa zao waliokuwa
wakisafiri kuelekea jiji la Constatine.
Taarifa zinasema kuwa wamepata mtu mmoja aliyenusurika huku waokozi wakiendelea kutafuta manusura zaidi.
Duru zinasema kuwa upepo mkali pamoja na hali mbaya ya anga ndiyo huenda ilisababisha ndege hiyo kuanguka.
Jeshi halijatoa taarifa yoyote mpaka sasa.
Ajali hii inasemekana kuwa mbaya zaidi kushuhudiwa katika mwongo mmoja na ya tatu ikihusisha ndege ya jeshi.
Ndege
nyingine ya kampuni ya Air Algerie Boeing 737, ilianguka punde baada ya
kuruka kutoka mjini Tamanrasset mnamo mwaka 2003,na mtu mmoja pekee
ndiye alinusurika.