HALI ya taharuki iliyoambatana na imani za kishirikina iligubika
Jiji la Arusha kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina kudondoka na
ungo wa kishirikina asubuhi ya Ijumaa iliyopita kisha ghafla
kubadilika kuwa kuku mweupe mwenye mayai ndani ya ungo, Uwazi limeona
mengi.
Mamia ya wananchi katika eneo la Kimandolu kando ya Barabara ya
Arusha- Moshi walimiminika kushuhudia tukio hilo lililojiri saa tatu
asubuhi.
Akizungumza na Uwazi, shuhuda mmoja wa tukio hilo ambaye ni dereva wa bodaboda, Martin Mbise alisema:
“Nilikuwa
kwenye shughuli zangu za kila siku, ghafla niliona kitu kipana
kikidondokea kwenye huu mtaro, ndani yake nikamwona mtu amekaa akiwa
uchi wa mnyama.
“Wengi tuliamua kusogelea eneo la tukio, lakini kabla hatujakifika,
mtu huyo alitoweka, badala yake mle mwenye ungo mkawa na kuku mweupe na
mayai zaidi ya kumi, tulishangaa sana:
Mbise alisema hali hiyo
ilidumi kwa saa mbili na nusu, ndipo wananchi hao wakaamua kumchoma moto
kuku huyo baada ya kumuua na kuyavunja mayai.
Hata hivyo, alisema haikuwa rahisi kuku huyo kuungua licha ya
kumwagiwa mafuta ya taa na petroli na wakachukua uamuzi wa kumkatakata
na kugawana nyama yake huku baadhi
yao wakikimbia hovyo na kulaani tukio hilo.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo walisema tukio hilo ni laana na
anapaswa kuitwa mtumishi wa Mungu kwa ajili ya kukemea pepo mchafu kwa
maombi ya kiroho wakiamini mchawi huyo alikuwa ana lengo la kuwadhuru
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Lebaratus Sabas hakuweza
kupatikana kuzungumzia tukio hilo, lakini baadhi ya maafande waliofika
katika eneo hilo walithibitisha.
