Monday, 16 December 2013

UJUE MTO RUVUMA AMBAO NI CHANZO KIKUBWA CHA MAPATO KWA JAMII INAYOISHI KANDO KANDO YA MTO HUO


Mto Ruvuma unavyo onekana kwa juu 

 Hawa ni Vijana wa Ruvuma maarufu kwa WAYAO  wakijitifautia ridhiki  katika mto Ruvuma , Kila pikipiki moja huoshwa kwa Shilingi Elfu moja(1000) wanapokuwa wanaosha mafuta husambaa katika maji . Je kwa hali hii kuna matumizi mazuri ya vyanzo vya mto Ruvuma ikiwa  mbele yake watu hutumia maji haya kwa matumizi ya nyumbani(kupikia na kunywa)   Pia mto huu huumwaga maji yake katika Mto RUVUMA
 
Hawa ni akina mama wakifua nguo katika mto huu wa Ruvuma na pembeni kukiwa na mtoto anayechezea maji ,pengine mtoto huyu uwenda akawa anachota kwa mikono yake na kunywa
 Hii ndiyo hali halisi ya chanzo cha  mto Ruvuma ulipo Ruvuma kwa WAYAO ukiwa umeanza kukauka maji kutokana na matumizi mabaya ya vyanzo vya maji kwa kupitisha mifugo kiholela na ulimaji pembezoni mwa mto,

 Bibi(MBUYA) akisuuza nguo baada ya kufua katika mto Ruvuma huku mjukuu wake akitelemka kumfuata ndani ya maji
 Vijana wakiwa kazini kuelekea katika kuvua samaki

Baadhi ya watalii pamoja na watu mbalimbali ambao ni wakazi wa pembezoni mwa mto huo wakitazama mambo mbalimbali pamoja na kununua Samaki

Hapo mwaka 1886, Askofu wa Kanisa la Anglikana, Charles Alan Smythies, alikuwa MZUNGU sio mtu wa Kwanza kuona chanzo cha mto RUVUMA. Inaelezwa kuwa Askofu huyu alifika katika chanzo cha mto Lujenda, naodaiwa kuwa chanzo muhimu cha mto Ruvuma.
Inasemekana kwamba wakati askofu huyo alipokiona chanzo hicho, uvumi ulienea miongoni mwa wenyeji kwamba kwa vile chanzo hicho kilikuwa na MASHETANI basi Askofu Smithies angekufa. Hata hivyo askofu huyo hakufa kama ilivyohofiwa.

Vile vile yafaa kukumbushana hapa kwamba Askofu Charles Allan Smithies ndiye alikuwa askofu wa kwanza wa UMCA (University Mission to Central Africa) – ya Anglikana visiwani ZANZIBAR hapo mwaka 1892

Mto Ruvuma  ni mto mrefu nchini Tanzania. Chanzo chake kiko mashariki ya Songea katika milima ya Matagoro upande wa mashariki wa Ziwa la Nyasa. Inaelekea magharibi kati ya vilima kwenye kimo cha 1000 m karibu na Songea inageukia kusini. Mdomo uko Bahari ya Hindi kati ya Mtwara (Tanzania) na Rasi ya Delgado (Msumbiji).
Mpaka kati ya Tanzania na Msumbiji inafuata mwendo wake kwa km 730.
Tawimito muhimu ni Muhuwesi na Lumesule upande wa Tanzania halafu Lucheringo na Lujenda upande wa Msumbiji.

Inaelekea magharibi kati ya vilima kwenye kimo cha 1000 m halafu inabadilika mwelekeo kwenda kusini; inapofika mpaka wa Tanzania na Msumbiji takriban 200 km baada ya chanzo inageuka tena kuelekea mashariki hadi bahari. 35 km baada ya kuungana na Lujenda pana maporomoko ya Upinde. 160 km kabla ya kufika mdomoni bonde la Ruvuma inapanuka kuwa na upana wa 10 km; lalio la mto ni karibu mita 500 likiwa na visiwa vya mchanga. Wakati wa ukama maji hupungua sana hadi watu kuvuka mto kwa miguu; wakati wa mvua umbali kati pande zote mbili unafikia zaidi ya kilomita moja.

Mdomo mwenyewe una umbo la delta. Athira ya maji kujaa au kupwa baharini huonekana 20 km kabla ya mdomo mwenyewe. Kabla kufika kwenye delta kuna feri inayobeba magari kati ya Tanzania na Msumbiji. Feri ilipelekwa hapa na mapadre Wabenedikto wanaofanya kazi pande zote mbili za mto.