Weekend
iliyopita msanii wa Tanzania Vanessa Mdee a.k.a Vee Money alikuwa
nchini Nigeria kwa ajili ya kuhudhuria na kutumbuiza katika show kubwa
ya mara moja kwa mwaka, ambayo huwakutanisha wasanii wa A-list wa nchi
hiyo katika jukwaa moja.Jukwaa la ‘Rhythm Unplugged’
Baada ya show hiyo Vanessa alipost picha Instagram akiwa na dancers wa Naija waliopanda naye jukwaani kumpa support na kuandika;
“These
ladies gave me LIFE tonight S/O to Nigeria’s CLIMAX dancers! What a
stage, what an audience, what a show, what a slayin!!!! THANKYOU
JESUS!!!!”.
Victoria Kimani
Naye
msanii wa Kenya mwenye makazi nchini Nigeria Victoria Kimani, kupitia
Instagram aliandika kuwa kati ya vitu alivyovipenda kwenye tamasha hilo
ni pamoja na show ya Vee Money ambaye ameiwakilisha vizuri Afrika
Mashariki.
“My
Favorite Part of the Show from Top Left: My Gals @ceodancers Killed it
as usual! @2faceidibia1 THE YOUNG LEGEND … Wycleff Jean Shut it Down!
And my girl @vanessamdee Made me Proud! She repped East Africa well
#Nigeria #Tanzania #Haiti #SouthAfrica #Kenya #RhythmUnplugged”
aliandika Victoria.
Rhythm
Unplugged ni show iliyofanyika Jumapili iliyopita Lagos, Nigeria na
kuwakutanisha wasanii wakubwa wa Naija katika jukwaa moja wakiwemo
2Face, P-Square, WizKid, D’Banj, Davido na wengine. Host wa show hiyo
kwa mwaka huu alikuwa nyota wa kimataifa Wyclef Jean.