Tuesday, 17 December 2013

Lulu akana kutoka na Young Dee

 

MSHINDI wa tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike ya iliyotolewa na  Zanzibar International Film Festival (Ziff), Elizabeth Michael ‘Lulu’,  amekanusha taarifa zilizozagaa kwamba anatoka kimapenzi na mwana  Hip Hop, David Genzi ‘Young Dee’.
Akizungumza na Mwanaspoti, Lulu amesema anashangaa taarifa hizo kusambaa kwa kasi wakati anadai kuwa hazina ukweli wowote.
“Inanishangaza kwa kweli, kwanza kabisa nilipigiwa simu na baadhi ya watu kwamba wamesikia tukio la mimi kufumaniwa, yaani wewe ni mtu wa 100 unanipigia, kila mtu ananiuliza kulikoni, nashangaa maana sijawahi hata kumfikiria Young Dee kimapenzi,” alisema Lulu.
“Halikadhalika yeye hajawahi kunitamkia jambo la aina hiyo japokuwa tumeshawahi kufanya kazi pamoja, ninavyokwambia sijawasiliana naye kama mwezi hivi, sasa hiyo tetesi sijui imetokea wapi maana hata aina ya gari wanalolitaja sijawahi kulimiliki.”


credit mwnaspoti