Shirikisho
la soka nchini Uganda limeandika barua kwenda FIFA likisaka ufafanuzi kuhusu
uhamisho wa mshambuliaji Emmanuel Okwi aliyeuzwa kutoka SC Villa kwenda Yanga.
Siku ya
jumatatu, Okwi alirirpotiwa kujiunga na mabingwa wa Tanzania bara klabu ya
Yanga kwa ada ya uhamisho wa $100,000 kwa mkataba wa miaka miwili, na huku huko
nyuma FIFA ilimuidhinisha Okwi kujiunga kwa mkopo na klabu ya SC Villa akitokea
klabu ya Tunisia Etoile du Sahel.
Okwi
ameichezea SC Villa katika ligi kuu ya Uganda kwa kipindi cha takribani miezi
miwili akiifungia timu hiyo mabao matatu.
“Tumeiandikia
barua FIFA kwa sababu tunahitaji watueleze kama uhamisho huo ni sahihi,"
alisema CEO wa FUFA, Edgar Watson.
Lakini
mkurugenzi wa SC Villa, Edgar Agaba, aliongea na mtandao wa mntfootball na
kusema kwamba mchezaji huyo alijiunga na klabu ya Yanga akiwa mchezaji huru.
Wiki
iliyopita shirikisho la soka Afrika kilisema kwamba Okwi na Godfrey Walusimbi
hawakuwa na uhalali wa kucheza kwenye michuano ya 2014 Africa Nations Championships (CHAN) kwa
sababu walikuwa na matatizo na vilabu vyao vya zamani Etoile du Sahel na Don
Bosco (DR Congo).
Itakuwa
jambo la kuvutia kuona namna Okwi, ambaye alizuiliwa kucheza CHAN, akiruhusiwa
kujiunga na klabu ya Yanga na huku akiripotiwa kuwa na matatizo na klabu ya
Etoile du Sahel.hili.” alisema Watson.