Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Mh.Ismail Aden Rage (MB) amesema klabu ya Simba imefanyiwa mchezo mchafu baada ya
klabu ya Yanga kumsajili mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Arnold Okwi.
Akizungumza na Jamii na Michezo Ismail Aden Rage amesema mpaka sasa kuna kesi tatu katika Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA),kesi ya kwanza ni simba na timu ya Etoile du Sahel ya Tunisia,kesi ya pili ni ya Etoile du Sahel na Okwi ambapo Etoile du Sahel wanalalamika kuwa tangu mwezi wa tano Okwi hajarudi Tunisia mara baada ya Shirikisho la Soka Uganda(FUFA)kumuamba akacheze katika timu ya taifa,na kesi ya tatu ni kwamba Okwi naye adai kuna malipo yake ambayo ajalipwa.
"kuna mambo mengi ambayo yanafanywa kwa ajili ya kunizorotesha mimi ,ingawa sina uhakika na inasemekana kuwa ni mipango ya ndani kwa baadhi ya viongozi wa simba kumpeleka Okwi katika klabu ya Yanga,ili wanachama waweze kuwa na hasira na mimi " amesema Rage
"katika misingi hii mitatu,tunashindwa kuelewa SC Villa wameingiaje hapo katikati na kuja kutoa uhamisho,kwaiyo sisi tayari tumeshawaandikia Tff barua kutaka maelezo ya kina,na pia tumeandika barua kwa FIFA kutaka maelezo ya kina,na bahati nzuri watu wa Etoile du Sahel wameandika barua kwa FIFA wakilalamika"alisema Rage
"Kuna barua ilikuwa imeletwa kutoka FIFA,ambayo ilikuwa imetupa muda wa siku kumi tuwe tumelipa milioni kumi,lakini kwa bahati mbaya iyo barua ilikuwa imekaa klabuni haijashughulikiwa,leo mimi nimeishughulikia asubuhi nimelipa milioni kumi FIFA,na FIFA wameahidi watachagua jaji ambaye atasimamia kesi yetu,ili haki ya Simba iweze kupatikana,sisi kikubwa tunachotakiwa ni kudai haki yetu kutoka FIFA"alifafanua Rage
Ismail Aden Rage amewaomba lidhaa wanachama wa simba ili awaze kuitisha mkutano mkuu wa uchaguzi mwezi ujao kwa ajili ya kuinusuru klabu hiyo.