KULIA NI Mkuu
wa Wilaya ya Tabora Mjini , Suleiman Kumchaya....(picha aihusiani na taarifa hii bali ni kukupa taswira tu)
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini , Suleiman Kumchaya, ameingia kwenye kashifa nzito ya kumtapeli mama mmoja fedha taslimu kiasi cha Sh. milioni 50.
Kumchaya ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke huyo
aliyejitambulisha kwa jina la Betty Matemba, anadaiwa kufanya utapeli
huo katika vipindi tofauti mara baada ya kushindwa ubunge 2010.
Akizungumza na gazeti hili, Betty alisema Kumchaya wakati akiwa
mbunge walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na walikuwa wakiishi kama mtu
na mumewe.
“Unajua huyu bwana alikuwa mshauri wa Rais Mkapa, baadaye aligombea
ubunge katika kipindi cha awamu ya kwanza ya serikali ya Rais Kikwete
na alishinda lakini awamu ya pili hakuweza kupata.
“Wakati akiwa ni mbunge, bado alikuwa na uwezo mdogo sana kifedha,
alinishawishi kumkopea fedha benki lakini siku zinavyokwenda mwenzangu
hata halipi deni ndiyo nikachukua uamuzi wa kwenda bungeni ili akatwe
marupurupu yake ya ubunge lakini ikaonekana hakuwa na hata senti mmoja,”
alisema Betty.
Kwa mujibu wa Betty, mkuu huyo wa wilaya alipomaliza kipindi chake
cha ubunge, maisha yake yakawa magumu kwani hakuwa na fedha wala mradi
ingawa alikuwa akimiliki mamia ya ekari.
“Anao uwezo wa kunilipa, anazo ekari 60 za mikorosho Mtwara
Vijijini, ekari 500 za ardhi huko Nachingwea akiziuza ni rahisi yeye
kunilipa lakini anachonifanyia ni uhuni.
Awali tulikubaliana anilipe fedha hizo ili nilipe madeni yote
ninayodaiwa,” alisema.
Akiwa na makabrasha yanayoonyesha michanganuo ya fedha alizomtapeli, Betty anasema baada ya kupata ukuu wa wilaya alianza kumlipa kidogo kidogo ambapo Juni 28 mwaka jana alilipa Shilingi milioni moja na Julai 31 mwaka jana, alilipa Shilingi milioni moja na baada ya hapo hakuendelea tena.
Akiwa na makabrasha yanayoonyesha michanganuo ya fedha alizomtapeli, Betty anasema baada ya kupata ukuu wa wilaya alianza kumlipa kidogo kidogo ambapo Juni 28 mwaka jana alilipa Shilingi milioni moja na Julai 31 mwaka jana, alilipa Shilingi milioni moja na baada ya hapo hakuendelea tena.
Alisema wakati fulani walishauriana yeye (Betty) na Kumchaya
wanunue vigari vidogo vya mizigo ili vimsaidie kusogeza maisha yake.
“Ilishindikana kununua hiyo gari kwani fedha ninayoitegemea ndiyo
hiyo… Jumamosi (jana) kuna uwezekano wa kuondolewa kwenye nyumba
niliyopanga Sinza kwani nimepandishiwa kodi na sina uwezo,” alisema na
kuongeza kuwa kodi ya mwaka anatakiwa kulipia Sh. milioni 3.6 na kwamba
mwenye nyumba tayari ameshamkabidhi barua ya kuondoka.
Betty alisema fedha hizo alitarajia kununua nyumba ambayo wakati
huo ilikuwa ikiuzwa Sh. milioni 70 lakini kutokana na ‘mheshimiwa’ huyo
kumrubuni, ilishindikana.
Alisema kutokana na jinsi alivyokuwa akimsumbua (Kumchaya) kulipa deni hilo, mkuu huyo wa wilaya alianza kutumia nguvu za giza.
“Kumchaya akiwa na mkewe mwingine Mpemba na rafiki yangu mmoja na
mumewe, walikwenda Mbagala kwa mganga wa kienyeji wakitaka kuniua au
kunifanya kichaa.
“Huyu mganga nilikuwa si mfahamu, lakini alipata namba yangu
akanipigia akitaka nimuone…nilikwenda na wifi yangu (dada yake
Kumchaya), tulipofika alinieleza yote pamoja na fedha aliyolipwa...,"
alisema.
Dada yake Kumchaya , alilipopigiwa simu kutoka Masasi, alikiri kutambua uhusiano uliopo wa Betty na Kumchaya.
“…huyu Betty ni wifi yangu kabisa, mkewe Selemani, ni wifi yangu ninayempenda sana.
Ni kweli Kumchaya na mkewe Fatma walikwenda kwa huyo mganga huko
Dar es Salaam wakitaka kumroga Betty.
Huyu mganga alimvuta Betty kimadawa hadi alipompata na siku hiyo tulikwenda wote kwa huyo mganga. Betty Mungu anampenda sana...," alisema Mwajuma kwa lafudhi ya Kimakonde.
Huyu mganga alimvuta Betty kimadawa hadi alipompata na siku hiyo tulikwenda wote kwa huyo mganga. Betty Mungu anampenda sana...," alisema Mwajuma kwa lafudhi ya Kimakonde.
Miongoni mwa fedha ambazo Betty anadai kuzikopa kwenye taasisi za
fedha kwa ajili ya kumridhisha Kumchaya ni pamoja na Shilingi milioni
saba (NMB), Shilingi milioni tisa (International Bank), Shilingi milioni
10 (Akiba Commercial) na Shilingi milioni 4.2 (Vission Saccos), hizo ni
mbali na zile alizokopa kutoka kwa watu binafsi.
“Ilifikia kipindi aliniomba nikope Sh. milioni tisa kwa ajili ya
kufanyia harusi ya mtoto wake, nilifanya hivyo na harusi ilikuwa nzuri
sana.
Nilipoona hana muelekeo wa kulipa madeni hayo ilibidi tuandikishiane,” alisema huku akionyesha nyaraka hizo.
Betty anasema pamoja na kumuitia wazee wa heshima na viongozi wa
dini ya Kiislamu ili wazungumze na Kumchaya alipwe deni lake,
ilishindikana kabisa.
“Mimi sina ugomvi na huyu bwana, ninachotaka anilipe deni langu tu ili tuishi kwa amani,” alisema.
Mkuu wa Wilaya, Kumchaya alipotafutwa kwa siku tatu mfululizo kwa
simu akiwa Tabora, alisema yuko kwenye kikao apigiwe baadaye lakini
alipopigiwa simu yake ilikuwa ikiita bila majibu.
“Unajua huyu mwanamke anakichaa…subiri niwasiliane na mwanasheria wangu nipigie baadaye,” alisema.
Hata hivyo, mwandishi wa habari hizi alipoendelea kumpigia simu yake ya mkononi, iliita bila majibu.
CHANZO:
NIPASHE