NAHODHA wa zamani wa England, David Beckham jana aliwafunika wenzake watano katika pati la uzinduzi wa filamu maalum iitwayo The Class of '92 inayohusu wachezaji sita wa zamani wa manchester Unitred.
Filamu hiyo ya Kiingereza inawahusu magwiji wa Manchester United: Beckham, Nicky Butt, Ryan Giggs, Gary Neville, Phil Neville na Paul Scholes.
Mke wa nyota huyo wa zamani wa Real Madrid ya Hispania, Victoria na watoto wake watatu wa kiume, Brooklyn, Cruz na Romeo waliungana nao na baba yao katika zulia jekundu mjini London.

Mtu wa familia: Beckham akiwa na vidume vyake, Brooklyn (nyuma katikati), Romeo (kushoto), Cruz (kulia) na mkewe Victoria katika zulia jekundu

Beckham akisaini autographs za mashabiki

Scholes (kulia) na familia yake

Giggs akipozi kwa ajili ya picha, siku mbili tangu asherehekee kutimiza miaka 40 ya kuzaliwa

Pamoja tena: The Class of '92 inaelezea historia ya Beckham, Butt, Scholes, Giggs na akina Neville ndani ya Manchester United

Kiungo wa zamani wa United, Butt na familia yake

Mwimbaji Harry Styles (kulia) akiwa na Beckham

Phil Neville, mkewe Julie na watoto wao, Harvey na Isabella

Nahodha wa zamani wa Arsenal, Tony Adams na mpenzi wake Poppy Teacher walikuwepo pia