Hapa wananchi wakiwachoma moto mbwa hao
Waitaka serikali kumuondoa OCD kwa kushindwa kulinda raia na mali zao
.DC aagiza hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika
……………………………………………………….
Na Bazil Makungu Ludewa na Nickson Mahundi
Wananchi
wa kata ya Ludewa wameungana pamoja kufanya maandamano ya kushinikiza
mbwa waliomuua mtoto na kumtafuna wanauawa baada ya mmiliki wa mbwa hao
kutishia kuwashtaki watakao husika kuwaua mbwa wake.Wakizungumza
kwa nyakati tofauti katika mkutano wa dharula ulioitishwa na Diwani wa
kata ya Ludewa Mama Monica Mchilo walisema Mbwa hao wamekuwa tishio kwa
muda mrefu kwani wameshateketeza mifugo mingi wakiwemo mbuzi lakini cha
kushangaza kila wanapolipeleka suala hilo katika vyombo vya dola mmiliki
huwaeleza walete ushahidi.Kutokana
na hali hiyo tata mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Madaha ameviagiza
vyombo husika ikiwemo idara ya kilimo na mifugo, jeshi la polisi
kuchukua hatua za kisheria kwa yeyote anayehusika na tukio hili akiwemo
mmiliki wa mbwa hao Bosco Thobias Lingalangala kwa sababu hakuna mtu
aliye juu ya sheria.
Juhudi
za kumpata mmiliki wa mbwa hao Lingalangala(BOLI) ambaye aliwahikuwa
kiongozi wa klabu ya yanga miaka ya nyuma hazikuzaa matunda kutokana na
simu yake kutopokelewa na baadaye kuzimwa kabisa.
Hali
hiyo imejitokeza tena kwa mmiliki wa mbwa hao alipoelezwa kuwa
wamefanya mauaji na kumla mtoto wa darasa la tatu katika shule ya msingi
Ludewa mjini aliyefahamika kwa jina la Ibrahim Chipungahelo(9)aliwataka
wananchi kuleta ushahidi licha ya kuwa Askari wa jeshi la polisi kwa
kutumia silaha na kuuokoa mwili wa mtoto huyo ukiwa tayali umeshaliwa
katika baadhi ya viungo.
Akiongea
katika mkutano huo mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Ludewa Bw.Omary
Kiowi alisema tukio na kauli za mmiliki wa Mbwa hao wawili Bw.Bosco
Lingalangala hazivumiliki kwa wanaludewa kwani amekuwa akiwatishia
wananchi kwa kutumia bastola kila wakati hivyo kikao hicho kiliamuru
mbwa hao wauawe na mmiliki achukuliwe hatua za kisheria.
“Tokea
nizaliwe zijawahi kuona Mbwa akitafuna mtu, hii ni mara ya
kwanza,hatuwezi kuvumilia na ninachokiomba wananchi msifanye fujo
naamini tukitoka hapa kwa kushirikiana na ofisi ya mifugo pamoja na
jeshi la Polisi tunakwenda kumuua mbwa aliyebaki na tunamtaka Bw.Bosco
atushtaki wananchi wote na Serikali yetu kwa sababu anadhani yeye yuko
juu ya sheria”,alisema Bw.Kiowi.
Kufuatia
kauli za vitisho wananchi wakaomba kikao kiahirishwe na kuanza
maandamano kuelekea katika nyamba ya mmiliki wa mbwa hao ambako aliuawa
marehemu Ibrahim na kuhakikisha wananmuua mbwa aliyebaki kwa kupigwa
risasi,kwa hasira walizo kuwa nazo wananchi hao waliamua kuondoka na
Mbwa hao wote wawili wakiwa wamekufa na kupita nao mitaani huku wakiimba
nyimbo mbalimbali.
Baada
ya kuzunguka na mizoga ya mbwa hao mitaani kwa muda mrefu hatimaye
walielekea katika ofisi ya kata na kuamua kuwachoma moto na kuwateketeza
kabisa na kuendelea na kikao ambacho kiliibua shangwe na vifijo baada
ya mzee Laurance Mtweve (Muhuchu) ambaye ni mzee mashuhuri kutoa kauli
ya kuutaka uongozi wa kijiji kumuandikia barua mkuu wa wilaya ya Ludewa
ya kufukuza Bosco kuishi eneo la Ikilu kutokana na vitisho vyake.
Mzee Muhuchu alisema kama uongozi wa wilaya utashindwa kufanya hivyo basi wazee wa wilaya ya Ludewa watamuandikia barua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kuwa wamechoshwa na unyanyasaji wa Bw.Bosco hiyo hawamuhitaji wilayani hapa tena.
Mzee Muhuchu alisema kama uongozi wa wilaya utashindwa kufanya hivyo basi wazee wa wilaya ya Ludewa watamuandikia barua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kuwa wamechoshwa na unyanyasaji wa Bw.Bosco hiyo hawamuhitaji wilayani hapa tena.
Alisema
kwani imekuwa kawaida yake kuwatisha wananchi kwa kutumia bastola hali
inayowafanya wananchi kuishi kwa kuhofia usalama wao kwani inaonekana
yuko juu ya sheria kutokana na kufanya matukio ya ajabu lakini
wanaoshtaki hupuuzwa na jeshi la polisi hapa Ludewa.
Aidha
Diwani wa kata ya Ludewa kupitia CCM mama Monica Mchilo aliwataka
wananchi kupunguza jazba wakati sheria inachukua mkondo wake ingawa
awali alionesha kutoridhishwa na kauli za mmiliki wa mbwa hao kuwa
atawashtaki watakaohusika kuwaua.
Mama
Mchilo alisema hakuna aliyeridhishwa na kauli mbaya za Bosco lakini
anaamini Serikali ni sikivu itasikia kilio cha wananchi wa kata ya
Ludewa kutokana na vitisho vya mtu huyo ambaye hana hata chembe ya utu
kwa kusema mbwa wasiuawe bali atawalipa fidia wafiwa.
Aliwashukuru
wananchi kwa kufanya maandamano ya amani ambayo hayakuleta madhara kwa
jamii lakini yalifanikisha kuwaua mbwa ambao walikuwa ni tishio kwa
jamii hasa kwa wanafunzi wanaopita eneo hilo ambako aliwafugia mbwa hao.