madai kwamba bunge hilo linafuja fedha za wananchi bila sababu ya msingi.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake wa kundi la ukawa Mwenyekiti wa chama cha NCCR mageuzi James Mbatia amedai kuwa hadi sasa bunge hilo halina mueleko na linafanyika kwa matakwa ya kundi moja hivyo masuala mengi yanayoendelea kujadiliwa na wajumbe wake hayataweza kuleta matokeo chanya ya katiba mpya inayohitajika na wananchi.
Naye Mwenyekiti wa chama cha wananchi- CUF, Prof. Ibrahim Lipumba amesema baadhi ya matumizi ya bunge maalum la katiba ni ubadhirifu wa fedha za umma
Aidha viongozi hao wa UKAWA wamesema wapo tayari kandamana na kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima kama Rais Kikwete hataweza kusitisha shughuli za bunge la katiba.
Wajumbe wa bunge la katiba wanaendelea na shughuli ya kupitia rasimu ya katiba kwenye kamati 12 za bunge hilo na watarejea bungeni Septemba pili mwaka huu.
Hata hivyo baadhi ya wajumbe wa bunge hilo wakiwemo wanaounda UKAWA wamesusia shughuli hizo za bunge kwa sasa kwa madai kuwa baadhi ya madai yao hayajapatiwa suluhu.