Friday, 11 July 2014

Kombe la dunia katika Vatican ?


Papa Francis na Papa Benedict kushabikia fainali ya kombe la dunia ?

Je ushawahi kushabikia smechi ya kandanda baina ya mahasimu wawili wa jadi ?
Sasa hebu fikiria Mashabiki wa mechi ya fainali kuwa ni Viongozi wa kidini .
Taswira hiyo huenda ikakamilika siku ya jumapili Papa Francis ambaye ni Raiya wa Argentina akitizama mechi baina ya Argentina na Ujerumani na Papa mtangulizi wake Benedicto 16 raiya wa Ujerumani.
Makao makuu ya Kanisa Katoliki hata hivyo imekuwa wazi ikisema kuwa hilo huenda lisikamilike kwani papa Benedicto sio shabiki sugu ukimlinganisha na papa Francis ambaye ni shabiki sugu wa Argentina.
Msemaji wa Vatican Federico Lombardi akisema kuwa labda kadinali mkuu wa zamani wa Buenos Aires Jorge Bergoglio yaani papa Franci atatizama fainali hiyo.
Argentina na Ujerumani zilichuana katika fainali ya kombe la dunia 1986
Papa Benedict XVI, 87, anajulikana kuwa msomi na pia mwenye uraidbu wa mziki wa ala mara nyingi akipapasa roho yake kwa kucheza piano .
Wangdani wa Vatican ahata hivyo wanasema kua katika enzi zake Papa Benedict XVI alikuwa hawezi kosa matokeo ya mechi za klabu anayoishabikia ya Bayern Munich.
Gazeti moja la Italia''the Osservatore Romano'' ndilo lililotibua uvumi huu lilipochapisha habari kabla ya kuanza kwa kombe la dunia lilipobashiri kuwa Argentina itakutana na Ujerumani katika fainali ya kombe la dunia na hivyo kushuhudia mashabiki wa haiba yake , papa Benedicto wa 16 na papa Francis .