STORI: MAKONGORO
“Ndugu
zangu, kufuatia maradhi ya ajabu yanayonisumbua sina raha ya maisha,
niheri ningewafuata wazazi wangu waliotangulia mbele ya haki
nikapumzike.“Nimekuwa mtu wa maumivu wakati wote, kulala na kula kwangu
ni shida tupu mbaya zaidi ndugu ninaoishi nao hawana uwezo.
“Naamini kama wangekuwa na uwezo huenda ningekuwa nimepona maradhi haya
yaliyoanza kama utani baada ya kunipeleka katika hospitali kubwa na
kupatiwa tiba ya uhakika, kwa kweli nateseka jamani!
“Naumia zaidi ninapowaona vijana wa umri wangu wakiwa wanasoma na wenye
furaha, wakati mimi nateswa na haya maradhi ambapo nisipopata tiba
hatima yangu itakuwa kifo.
“Kabla ya kuanza kuugua, nilikuwa naishi na wazazi wangu huko Majengo, mkoani Tanga, bahati mbaya mwaka 2000 walitengana.
“Kufuatia
kutengana kwao, mama alinichukuwa tukaja hapa jijini Dar kwa mama
mkubwa tukaanza maisha mapya bila baba.“Tukiwa tunaendelea na maisha,
Desemba mwaka huo, mama mkubwa aliugua na kufariki dunia, kifo chake
kilikuwa pigo kubwa kwetu kwani tulikuwa tukimtegemea kwa kila kitu.
“Kufuatia tuliyekuwa tukimtegemea kufariki, mimi na mama tulianza kuishi
maisha ya kubangaiza, ilipofika Mei 21, 2002 mama naye akafariki dunia
baada ya kuuguwa kwa muda mfupi.
“Nilibaki peke yangu, babu alinichukuwa tukaenda kuishi Banana, Ukonga
lakini haukupita muda mrefu aliugua na kufariki dunia na kuniacha nikiwa
darasa la tano katika Shule ya Msingi Kitunda.
“Baada ya babu kufariki, nilikosa pa kuishi ilibidi nichukuliwe na babu
mwingine aliyekuwa akiishi Korogwe, Tanga. Hata hivyo, babu huyo hakuwa
na uwezo kwani alikuwa mzee sana, alifariki akiwa na umri wa miaka 78.
“Wakati babu anakufa ndipo nilianza kupata uvimbe kiunoni kwa nyuma.
“Awali nilidhani ungeisha lakini kadiri siku zilivyosonga mbele uliongezeka.
“Nikawa napata maumivu makali na kushindwa kujisaidia haja ndogo, kwani
mkojo ulikuwa hautoki. Siku moja nilikwenda kwa mwenyekiti wa kijiji
chetu cha Mgombezi ili anisaidie matibabu. Aliniandikia barua ya kuomba
fedha kwa watu lakini sikufanikiwa.
.....akizidi kuonyesha kwa ukaribu.
“Nilipoona
hali si nzuri na sina fedha, niliamua kwenda Hospitali ya Wilaya
Korogwe (Magunga), nikalazwa kwa wiki mbili. Walitoboa tumbo na
kuniwekea mpira wa kutolea haja ndogo, cha kushangaza maumivu yakazidi
kuwa makali zaidi.
“Ndipo mtoto wa marehemu mama mkubwa, Salha Magamba alisikia kilio
changu akanitumia nauli na kuja tena hapa kwake Dar.“Nilimkuta anaishi
maisha duni kwa kutembeza biashara ya mkononi huku akiishi katika chumba
kimoja na mwanaye. Mei 14, mwaka huu alinipeleka Hospitali ya Taifa
Muhimbili kutibiwa ambapo madaktari waliangalia jinsi ya kuweka mpira
vizuri. Wakati huo uvimbe nao ulikuwa mkubwa karibia kilo mbili na nusu.
“Nililazwa Jengo la Kibasila Wadi ya 14, nilifanyiwa kipimo cha CT Scan
lakini vipimo vingine niliambiwa vibovu. Dada alinipeleka Hospitali ya
Tumaini (Dar) ambapo kipimo kilikuwa shilingi 200,000 kwa hiyo
sikufanyiwa kwa kukosa fedha hizo.
“Kuanzia hapo nimekuwa nikibadilishiwa mpira kila baada ya wiki mbili
kwa shilingi 30,000. Kwa upande wa uvimbe mgongoni ambao unaniuma kupita
kiasi bado matibabu yake kwani nasubiri majibu, sijui itakuwa shilingi
ngapi!”
Ndugu
msomaji, bila shaka umesikia kilio cha kijana Twaha. Kwa kifupi
anahitaji sana msaada ili kuokoa maisha yake. Kama umeguswa msaidie
fedha kupitia namba 0713-970 491 au 0789-288 743.