KOCHA
mpya wa Yanga SC, Mbrazi Marcio Maximo Barcellos, amesema timu hiyo
itatisha katika Ligi Kuu ya Bara na michuano ya Afrika chini yake.
Kocha
huyo wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars
aliyezaliwa Aprili 29, mwaka 1962, amesaini mkataba wa miaka miwili kwa
ajili ya kuifundisha timu hiyo akirithi mikoba ya Mholanzi Hans van der
Pluijm.
WASIFU WA MAXIMO:
JINA: Márcio Máximo Barcellos
KUZALIWA: 29 April 1962 (age 52)
ALIKOZALIWA: Rio de Janeiro (RJ) Brazil
TIMU ALIZOFUNDISHA:
Klabu ya sasa: Yanga SC
Timu Mwaka
1992-1993 Brazil U20
1992-1993 Brazil U17
1992 Mesquita
1994 Barra da Tijuca FC
1994 Qatar U20
1995 Al-Ahli
2002 Cayman Islands
2003 Livingston
2006-2010 Tanzania
2012 Democrata-GV
2013 Francana
Tangu Juni 27, 2014; Yanga SC
Mbrazil
akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo mjini Dar es Salaam,
amesema pamoja na changamoto ambazo anatarajia kuzipata kutoka timu
pinzani wa Yanga, kama Azam FC, Simba na Mbeya City, lakini
atahakikisha anajenga msingi bora ya soka itakayowezesha kutimiza
majukumu yake vizuri.
Amesema anataka kuona timu inashinda mechi zake za ndani ya nchi na nje, kwani anaamini Yanga ni klabu kubwa barani Afrika.
“Nataka
kuibadilisha soka ya Yanga ili liweze kufikia katika kiwango wa
kimataifa na hili linawezekana, kwani nani alikuwa anaijua TP Mazembe ya
DRC, lakini kwa kuwa iliandaliwa na kufanyika uwekezaji sasa ni klabu
kubwa Afrika” amesema Maximo.
Maximo
amesema, atahakikisha anajenga soka ya vijana kwa kuwa ni msingi wa
soka inapoanzia ambapo atakuwa na timu zenye umri tofauti.
Amesema, kikubwa anatarajia kuona jitihadi za wachezaji wa timu hiyo ndani ya uwanja, kwani kitu muhimu kwake ni ushindi.
Maximo,
pia atakuwa ni Mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo, akisaidiwa na Mbrazil
mwenzake Leornado Neiva ambaye atafundisha timu ya vijana waliochini ya
umri wa miaka 20, aliyesaini mkataba wa miaka miwili juzi.
Neiva pamoja na kuwa na kocha wa vijana atamsaidia Maximo katika majukumu yake katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Maximo
akiwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’
aliyeifundisha kuanzia mwaka 2006-2010, aliwahi kumleta wasaidizi wake
kutoka Brazili, ambao ni Markus Tinoco, ambaye alikuwa kocha wa timu ya
vijana waliochini ya miaka 20.
![]() |
Maximo na Msaidizi wake, Leonardo Neiva Martins kulia |
Lakini
Yanga wanatarajia kumwajiri kocha mwingine mzawa na kuwa wanne
akiwemo kocha wa makipa, Juma Pondamali kwa lengo la kuleta ufanisi
zaidi.
Katika
hatua nyingine, Maximo alisema anatarajia kuanza programu ya mazoezi
Jumatatu ijayo kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.
Maximo
aliyezaliwa mjini Rio de Janeiro, alikuwepo kwenye mabenchi ya Ufundi
ya timu za taifa za vijana za Brazil chini ya umri wa miaka 17 na 20
kuanzia mwaka 1992 hadi 1993.
Vikosi
hivyo ndani yake vilikuwa vina wachezaji walioibuka nyota wakubwa
Brazil baadaye kama Ronaldo Lima na Ronaldinho Gaucho, ambaye wote sasa
wamestaafu baada ya kuwika hadi kuwa Wanasoka Bora wa Dunia.
Kabla
ya hapo, mwaka 1992 alifundisha Mesquita, 1994 Barra da Tijuca FC za
kwao Brazil, 1994 akainoa U20 ya Qatar na mwaka 1995 akafundisha
Al-Ahliya huko.
Alifanya
kazi pia kama Mkurugenzi wa Ufundi wa viswia vya Grand Cayman kwa miaka
mitatu ambako alikataa ofa ya kuongeza mkataba kwa miaka 10 ili
akajiunge na Livingston FC ya Scotland Juni 5 mwaka 2003, alikosaini
Mkataba wa mwaka mmoja na kuwa kocha wa kwanza Mbrazil kufundisha timu
ya Uingereza.
Pamoja
na hayo, mambo hayakumuendea vizuri huko, baada ya mechi tisa
akiambulia ushindi wa mechi tatu, sare tatu na vipigo vitatu, akajiuzulu
Oktoba 14.
Juni
29 mwaka 2006, Maximo akasaini Mkataba wa kuifundisha Taifa Stars
ambayo mwaka 2009, aliiwezesha kufuzu kucheza fainali za kwanza za CHAN
nchini Ivory Coast.
Maximo
alijiuzulu kuifundisha Taifa Stars mwaka 2010, akiwaacha Watanzania
bado wanampenda- akaenda Democrata ya nyumbani kwao, Brazil.
Alifukuzwa
katika timu hiyo Februari 13 mwaka 2012 na Juni mwaka huo huo
alikaribia kujiunga na Yanga SC kurithi mikoba ya Mserbia, Kosta Papic,
lakini wakashindwana dau na klabu hiyo ikamchukua Mbelgiji, Tom
Saintfiet.
Novemba 2012, akajiunga na Francana ya kwao Brazil ambako ndipo anatokea sasa kuja Yanga SC baada ya kumaliza Mkataba wake.