Awali, kikosi kazi cha kufichua maovu cha Global Publishers (OFM), kilipewa malalamiko juu ya
dispensari hiyo kuwa ni kinara wa mchezo huo mchafu wa kuwatoa mimba mabinti wadogo hususan wanafunzi wa shule za msingi.
Siku aliyonaswa, ilikuwa majira ya jioni ambapo kaka wa mwanafunzi (jina tunalihifadhi) aliandaa mtego wa kumnasa daktari huyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa rafiki wa mdogo wake kuhusu mchezo huo mchafu anaoufanya daktari huyo.
Kaka huyo aliwapigia simu makamanda wa OFM ambapo walitia timu sambamba na polisi kwenda kuweka ‘kambi’ katika dispensari hiyo kuhakikisha tukio zima linakuwa ‘recorded’.
Kaka huyo alitanguliwa katika dispensari hiyo na kubana sehemu kumsubiri mdogo wake huyo afike ‘kutoa mimba’ huku makamanda wa OFM wakiwa wameseti mitambo yao maalum katika kila engo ya eneo hilo.
Majira ya saa tisa, mwanafunzi huyo alifika hapo akiwa ameongozana na kijana mmoja aliyesetiwa kuwa mpenzi wa mwanafunzi huyo na kuongea jambo (kumpa fedha) na daktari akiingia chumbani akiongozana na mwanafunzi huyo huko akiwa na vifaa maalum vya kutolea mimba.
Nesi,dokta chini ya ulinzi.
Baada ya kusubiri kwa dakika tano, kaka wa mwanafunzi huyo na
makamanda wa OFM waliingia katika chumba hicho na kumkuta daktari huyo
akiwa katika pilipilika za kumtoa mimba mwanafunzi huyo ambaye alikuwa
amelala chali.OFM ilifanikiwa kunasa meseji mbalimbali za daktari huyo zilizokuwa zikielekeza namna ya kufanikisha zoezi hilo la utoaji mimba.
Majirani ambao walishuudia tukio hilo walipongeza sana OFM kwa kumnasa daktari huyo kutokana na kukithiri kwa tabia hiyo dispensarini hapo.
”Jamani mmefanya vizuri sana kuja kukomesha mchezo huu hapa tumelalamika sana lakini hatusikilizwi,” alisema mzee mmoja aliyejitambulisha kwa jina la mzee Hamisi.
Daktari huyo alipelekwa katika kituo kidogo cha polisi cha Buguruni kisha kuchukuliwa maelezo ili hatua zaidi za kisheria dhidi ya daktari huyo ziendelee.
Mpaka timu ya OFM inaondoka eneo la tukio hilo, walimuacha daktari huyo akiwa anashikiliwa kituoni hapo na shauri lake likisomeka MNY/RB/336/2014.