Uhalali wa Bunge la Katiba Bila Hati halisi ya Muungano
Wajibu wa Vijana kwa Taifa ni Kuleta Tija kwa Taifa na Kuwezesha Vijana wengine wasio na fursa kulinganisha na fursa tulizo nazo. Wajibu wangu nikiwa Kijana ni kuhakikisha Taifa hili linaendelea kukua kiuchumi, kijamii na kisiasa bila kuathiriwa na historia mbaya yoyote lakini ikibebwa na historia yote nzuri.
Wajibu wa Vijana kwa Taifa ni Kuleta Tija kwa Taifa na Kuwezesha Vijana wengine wasio na fursa kulinganisha na fursa tulizo nazo. Wajibu wangu nikiwa Kijana ni kuhakikisha Taifa hili linaendelea kukua kiuchumi, kijamii na kisiasa bila kuathiriwa na historia mbaya yoyote lakini ikibebwa na historia yote nzuri.
Tanzania ni Jamhuri ya
Muungano uliotokana na maungano ya nchi mbili Tanganyika (Tanzania Bara)
na Zanzibar tarehe 26/04/1964. Mchakato wa muungano huu ulihusisha
shughuli nyingi na matukio mengi kabla, ndani ya mchakato wakati wa
kuunganika na baada ya kuunganika.
Historia ya mahusiano ya
nchi hizi mbili inakwenda miaka mingi nyuma mwanzoni mwa 1800 enzi za
biashara ya Utumwa. Mpaka mwaka 1860 dola ya Zanzibar ilikuwa ni dola
tajiri kuliko zote Afrika Mashariki kutokana na biashara ya Watumwa na
Pembe za ndovu. Watumwa na Pembe za Ndovu zilitoka maeneo ya Tanzania
bara ya sasa. Harakati za kudai uhuru wa Zanzibar mwishoni mwa karne ya
19 (miaka ya 1950), Tanganyika ilihusika kwa kiwango kikubwa sana. Mfano
katika Mkutano wa kuanzisha chama cha Afro Shirazi Party uliofanyika
kati ya tarehe 1 hadi 5 February, 1957, mkutano huo ulifanyika nyumbani
kwa Sheikh Abeid Amani karume na katika Mkutano huo alikuwepo Mgeni
Mwalikwa Rais wa TANU, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Katibu Mkuu
wa TANU Ndugu Zuberi Mtevu. Hii ni sehemu tu ya Historia ya mahusiano ya
waasisi hawa wa Muungano tangu wakati Mataifa haya yakiwa bado ni
makoloni.
Tarehe 10 December, 1963
Zanzibar ilipata Uhuru kwa ajili ya Sultan ambapo waafrika walio wengi
waliendelea kuwa chini ya umangimeza wa kisultani hadi tarehe 12
January, 1964. (Waafrika walivumilia kwa mwezi mmoja) na walipofika hiyo
siku wakafanya Mapinduzi Matukufu yaliyoiweka Zanzibar huru. Uhuru wa
1963 ulitolewa kwa ZNP/ZPPP.
Vyama hivi viwili
viliwakilisha tabaka la juu la wanyonyaji miongoni mwa matabaka ya
watawaliwa. Vyama vilitetea kubaki usultani, kutambuliwa rasmi Sultan
kuwa ni Mkuu wa Dola ya Zanzibar chini ya himaya ya Uingereza na
havikupigania kuondoa matabaka na unyonyaji katika jamii. Ni ASP pekee
ndiyo ilipinga kabisa kuendelea kuwepo kwa usultani baada ya Uhuru na
kudai usawa katika nyanja za kiuchumi, Kijamii na Kisiasa.
Uhuru Bandi kwa ZNP/ZPPP
ulipelekea kuwepo chuki miongoni mwa wanachama wa ZNP jambo lilopelekea
kuundwa kwa chama cha UMMA ambacho kilikufa baada ya Mapinduzi ya mwaka
1964 na wanachama wake wote kujiunga na ASP. Hivyo ieleweke wazi,
Mapinduzi ya mwaka 1964 yalikuwa dhidi ya SULTAN na WAAFRIKA VIBARAKA
waliotumika Kuwanyanyasa Waafrika Wenzao wakiongozwa na Sheikh Muhammed
Shamte (Waziri Mkuu). Historia ni ndefu tutatumia muda mrefu kueleza
hayo.
Uwepo au Kutokuwepo kwa
Hati ya Muungano kwa sasa hakuna Mantiki. Muungano huu ulitokana na
mahusiano ya muda mrefu na changamoto za kiutawala na hatari iliyokuwa
inaikabili Zanzibar baada ya Mapinduzi. pia Tanganyika ilikuwa ndiyo
taifa limetoka kupata Uhuru kwa miaka mitatu tu. Hivyo yote yalifanyika
kwa nia njema ya kulinda uswa na ustawi wa watu na mataifa yao.
Leo kudai hati,
hakutaongeza wala kupunguza maana ya Muungano. Maridhiano ya makubaliano
ya Muungano yalifikiwa kwa sheria namba 22 ya mwaka 1964 iliyosainiwa
April, 25 na Marais wa Pande hizi mbili za Muungano. Sheria hiyo
ilisainiwa kuafiki matendo yote waasisi hawa waliyoyafanya mfano
Utiaji wa Saini na Ubadilishanaji wa Hati za Muungano;
Uchanganyaji Udongo wa nchi husika
Mikutano mbalimbali ya viongozi hawa
Na yale yote waliyoafikiana kikanuni na kisheria sasa, kilicholeta uhai wa Muungano ni kukamilisha Dili kwa kuutangaza tarehe 26/4/1964.
Uchanganyaji Udongo wa nchi husika
Mikutano mbalimbali ya viongozi hawa
Na yale yote waliyoafikiana kikanuni na kisheria sasa, kilicholeta uhai wa Muungano ni kukamilisha Dili kwa kuutangaza tarehe 26/4/1964.
Sote Tumeapa kwa huo
Muungano na kwa tafsiri tu kuwa Muungano upo na ulikuwepo. Tunayoweza
kujadili ni mambo yaliyoko katika Muungano na si Kujadili Makaratasi ya
Muungano. Kwa uthibitisho wa kuwa matukio haya yalikuwepo,
Tutaambatanisha na Picha kadhaa za Mwalimu Nyerere na Sheikh karume
katika matukio mbalimbali kuelekea katika Utekelezaji wa masharti
waliyoyaweka katika Muungano.
Mwisho! Niwaase wajumbe
wenzangu, tuendelee na mjadala wa Katiba Mpya kwa Kutumia Rasimu, Kama
kuna hoja ya msingi sana kuhusu Mchakato huu, basi iwekwe mezani si
kuweka viashiria vya sababu.
Katibu Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM - 2014