Kikosi cha zimamoto kikiizima helkopta hiyo ya Jeshi la Wananchi Tanzania iliyokuwa imewabeba viongozi wa serikali.
MAKAMU
wa Rais Dk. Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky
Sadick, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
na mpiga picha wa TBC, George Kasembe wamenusurika kifo baada ya
helkopta waliyokuwa wanasafiria kupata ajali Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere.Viongozi hao walikuwa katika helkopta ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa ziara ya kukagua athari za mafuriko jijini Dar es Salaam.
Baada ya ajali, viongozi hao wamepatiwa matibabu katika majeraha waliyoyapata na wameendelea na ziara yao!
Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick,.