Stori: OFM YA GLOBAL PUBLISHERS
MARA nyingi manesi wamekuwa wakishiriki katika matukio mbalimbali ya kuua watoto wachanga na kutegemea kulipwa ujira kutokana na kazi hiyo.
Matukio mengi ya aina hiyo yamekuwa hayaripotiwi kutokana na usiri wa wahusika kutaka mambo yao yasiwekwe hadharani lakini Oparesheni Fichua Maovu (OFM), inaendelea kufichua unyama huo na kuumwaga hadharani.
Mara kadhaa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, chini ya Waziri Sophia Simba imekuwa ikikemea tabia mbaya ya baadhi ya manesi kutumia vibaya taaluma yao na kuendeleza mauaji hayo.
SAFARI HII NI MBAGALA
Baadhi ya wazazi wanaoishi Mbagala Kizuiani jijini Dar waliochoshwa na tabia ya manesi kuua vichanga, walipiga simu OFM na kulalamikia vitendo vilivyokithiri vya utoaji mimba katika dispensari iliyopo maeneo yao.
“Manesi wa kike wanafanya shughuli za kuua vichanga ambavyo bado havijapata ruhusa ya kuingia duniani, kwa kweli inauma sana,” alisema mmoja wa wazazi hao.
Taarifa zikasema kwamba manesi hao wapo wengi lakini anayefahamika zaidi ni Maria ambaye amejizolea umaarufu kwa kazi hiyo katika eneo lote la Mbagala.
“Ni muda mrefu amekuwa akifanya mchezo huo, tena anafanya shughuli zake bila ya hofu utadhani vitendo hivyo vimeruhusiwa na mamlaka husika,” aliongeza mzazi mwingine.
Badhi ya vifaa vilivyoandaliwa na nesi kwa ajili ya zoezi la utoaji mimba.
OFM IMEJENGA HESHIMAWazazi hao wamesema kuwa wanaamini kuwa Maria atanaswa kama alivyonaswa Dokta Mambo wa Kawe jijini Dar ambaye naye alikuwa maarufu kwa shughuli kama hizo lakini OFM ikamshikisha adabu.
Baada ya kutoa maelezo hayo, mmoja wa wazazi hao alitoa namba ya simu ya Maria kwa kamanda mkuu wa OFM.
MTEGO WAANDALIWA
Kamanda Mkuu wa OFM alimpigia simu Maria na kumwambia kuwa alikuwa akitaka huduma ya kumtoa mimba mke wa mtu aliyempa kwa bahati mbaya kabla mumewe hajarudi kutoka safarini.
Maria: Hakuna shaka wee njoo tu dispensari kwetu, si umeelekezwa?
Kamanda: Ndiyo.
Maria: Njoo basi tumalize kazi leoleo.
Kamanda: Hiyo kazi inaweza kufanyika kwa ufasaha?
Maria: Miye huwa sishindwi na chochote, wee njoo utafurahi kwa huduma yangu lakini wahi kwani namaliza shifti jioni.
Baada ya maelezo hayo, kamanda wa OFM akaanza kuwapanga vijana wake kwa ajili ya kumnasa Maria katika mtego huo siku hiyohiyo ya Machi 15, mwaka huu.
Mmoja kati ya vijana waliopangwa katika zoezi hilo ni mwanamke mjazito ambaye alitolewa hofu kwamba mimba yake haitatolewa na OFM watakuwa wameshavamia katika chumba cha utoaji mimba.
Pia, OFM iliwasiliana na polisi wa Kituo cha Mbagala Kizuiani kwa lengo la kumkamata Maria.
MCHEZO MZIMA
Saa tisa mchana, OFM walikuwa wametanda katika dispensari husika wakiwa na askari waliokuwa wamevaa nguo za kiraia.
KAMANDA ATINGA FRONTI
Baada ya kupeana ishara za kikazi, OFM na baadhi ya polisi waliingia ndani ya dispensari hiyo kwa nyakati tofauti huku wakijifanya ni wagonjwa.
NESI MARIA AITWA MAPOKEZI
Kamanda wa OFM alipofika mapokezi ya dispensari hiyo, alipokewa na kusema shida yake ilikuwa ni kuonana na nesi Maria.
Bila ya kinyongo wafanyakazi wa mapokezi waliwasiliana na Maria ambaye naye alimtuma msaidizi wake aitwaye Maimuna kuwapokea wageni hao kisha kuwapeleka katika chumba maalum.
Maimuna alizungumza na kamanda na kuanza kuelewana kuhusu malipo ya kazi hiyo ya utoaji mimba.
Maimuna: Huwa tunatoa huduma hiyo kwa shilingi 80,000.
Kamanda: Dah! Miye nina shilingi 50,000.
Maimuna: Ongeza kidogo maana ni kazi ngumu sana.
Kamanda: Naomba mnisaidie tafadhali.
Baada ya maongezi ya muda mrefu, Maimuna alikubali kupokea shilingi 50,000 na kuanza kumpima


