Akizindua rasmi Bunge maalaumu la Katiba
jana mjini Dodoma aliwataadharisha wajumbe wa Bunge hilo kuwa makini
kabla ya kuchukua uamuzi ambao unaweza kusababisha nchi kuingia kwenye
hatari "Hii Serikali isiyo na uwezo, tegemezi ambayo haina dhamana,
itakuwa inasimamiwa na wanajeshi ambao wakishindwa kulipwa mishahara
baada ya miaka mitano wakavua magwanda na kupindua nchi" Alionya.
Hata hivyo alisema "Watakachoamua
Watanzania ni hichohicho wakiamua mbili tutakwenda huko huko, wakiamua
tatu tukwenda lakini kweli serikali hii itasimama?.Alihoji na kuongeza
"Suala la mfumo wa serikali tatu si jambo dogo ni lazima wawe makini
kuamua.
