Friday, 28 March 2014

TAARIFA MPYA KUPOTEA KWA NDEGE YA MALASYIA AIRLINES

Ndege 9 za kijeshi na Moja ya kiraiya zinatafuta mabaki ya ndege ya Malaysia ya MH370.
Maafisa wanaosaidia katika harakati za kuitafuta ndege ya Malaysia ya MH370 iliyopotea majuma tatu yaliyopita , wametangaza kuwa wanabadilisha eneo la kuitafuta mabaki ya ndege hiyo.
Eneo hilo jipya litakuwa kilomita elfu moja mia moja kazkazini mashariki mwa kusini mwa bahari hindi.
Mamlaka ya usalama wa baharini nchini Australia imesema kuwa hatua hiyo inatokana na taarifa muhimu na utafiti wa Malaysia pamoja na matokeo ya utafiti wa rada ya ndege hiyo iliyotoweka.