KOCHA
Sir Alex Ferguson amepokea Shahada ya heshima kutoka Chuo Kikuu cha
Ulster jana kutokana na mchango wake mkubwa katika soka.
Kocha
huyo wa zamani wa Manchester United, ambaye alistaafu mwishoni mwa
msimu uliopita baada ya miaka 26 ya kuwa kazini Old Trafford, alipokea
Shahada ya heshima ya Daktari wa Sayansi (DSc.) kutoka kwa mwigizaji na
mshauri wa Ulster, James Nesbitt.
Mwalimu
huyo mwenye umri wa miaka 72 alikwenda Ireland Kaskazini kwa ajili ya
shughuli hiyo, ambayo ilihudhuriwa na zaidi ya watu 500, hususan
wanafunzi na wahitimu.
Ferguson akiwahutubia wanafunzi baada ya kupokea tuzo yake Chuo Kikuu cha Ulster
Wakati wa furaha: Sir Alex Ferguson alipopokea Shahada yake ya heshim jana
