 |
Wakazi
wa Dar es Salaam pamoja na wahudumu wa bar ya Bulls park wakimuangalia
kijana ambaye jina halikufahamika akiwa amelala chini baada ya kuzidiwa
na pombe.Kijana
mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja alijikuta akianguka na
kutokwa na povu mdomoni kwa kile kinachosemekana kwamba alizidiwa na
pombe.
Nkurlu
Exclusive ilifika mda mchache eneo la tukio na kushuhudia kijana huyo
akiwa amelala chini pasipo kujiweza. Wasamaria walionekana kujaribu
kumwagia maji ili aweze kurudi katika fahamu zake pasipo mafanikio.
Kama
baada ya dakika 10 alitokea kijana mmoja na kukiri kuwa ndiye aliyekuwa
akistarehe nae, alieleza hali halisi na kusema kabla ya kuanza kunywa
pombe kijana mwenzake alipata mlo wa nguvu tuu kisha ndo wakaanza
kushusha mbili tatu. Alisema wakati wakuondoka alimkabidhi kwa dereva
bajaji mmoja ila hakufanikiwa kupanda ile Bajaj na kukuta amedondoka. Kijana
huyo pia alisema kuwa kijana mwenzake alikuwa ni mwenyeji wa Mwanza na
alikuja Dar es Salaam maalumkwa ajili ya kujirusha na nayeye na ndipo
akakutwa na huo mkasa. |
 |
| Kijana
ambaye jina lake halikufahamika akiwa amedondoka chini mara baada
yakuzidiwa na pombe eneo la survey jijini Dar es Salaam. |
Rafiki yake na kijana aliyendondoka(mwenye t-shirt nyeupe kushoto) akijaribu kuwasiliana na ndugu wa mwenzake.
*Wadau tujifunze kunywa pombe bila kupita kiasi maana ni hatari*