Friday, 21 March 2014

NADIR HAROUB, AMEJIIMARISHA NA KUIMAIRISHA SAFU YA ULINZI YA YANGA SC




Na Baraka MbolemboleMchezaji anatakiwa kupiga hatua siku zote katika uchezaji wake.
Unapopewa jukumu kama nahodha wa timu, linakuwa ni jambo la changamoto nyingine na linachangia kumfanya mchezaji kuwa bora, na ni kitu ambacho kinaweza kumfanya mchezaji kubadilika katika uchezaji wake kiujumla. 
Kama nahodha unakuwa na kiwango kisichobadilika, hasa katika
kupandisha kiwango cha uchezaji, watu watakusema kwa namna
wanavyotaka.

Kiwango cha sasa cha nahodha wa timu ya Yanga SC, Nadir Haroub kimeonekana kuimarika na kupanda. Wakati, Yanga ilipocheza michezo miwili dhidi ya Al Ahly ya Misri, katika ligi ya mabingwa Afrika, mapema mwezi huu na kuruhusu bao moja katika muda wa dakika 180, safu ya ulinzi ilionekana kucheza kwa umakini mkubwa huku, Nadir na Kelvin Yondan wameonekana kucheza kwa maelewano mazuri.

Unapobadilishiwa mtu wa kucheza nao kama beki wakati mwingine
linapelekea mchezaji kupata wakati mgumu kutokana na mazoea ambayo mara nyingi hujenga uimara wa beki kama safu muhimu ya timu. 
Nadir, amekuwa akicheza sambamba na Kelvin kwa msimu wa pilisasa, lakini kiwango chao wakicheza pamoja katika michezo dhidi ya Mtibwa Sugar na Azam FC, na namna ubadilikaji wa walinzi mchezo ni mzuri tofauti na walivyokuwa wakicheza katika siku za nyuma.

Hakuna kitu kigeni katika soka. Wakati mwingine mchezaji unatakiwa kuzoea kucheza tofauti na mchezo uliouzoea kutokana na msaidizi wako anavyokuwa akitimiza majukumu yake. Nadir ameonekana kupunguza makosa yake ya kuondoka mara kwa mara katika eneo lake la muhimu, kwa kuachana na stahili yake ya kucheza kwa kumfuata mshambuliaji wa timu
pinzani. 
Kama, Namba Tano, Nadir anatakiwa kucheza kwa kuwaongoza
wasaidizi wake huku yeye akicheza kwa kusahihisha makosa yanayokuwa yanafanywa na wenzake.

Katika umri wa miaka 31 sasa, mchezaji huyo ameonekana kutulia chini ya kocha, Hans. Kuwa nahodha inasaidia kujenga mtazamo wa ushindi muda wote kwa mchezaji. 
Kama unakuwa nahodha na huna sifa hizo si kitu kizuri, Nadir ni mchezaji mwenye usongo wa kupata ushindi uwanjani.

Wakati mwingine beki unapitwa na timu inafungwa, ni kitu ch
a kawaida. Lakini ni lazima kufanya jitihada kuzuia hilo kadri
iwezekanavyo. 
Mlinzi makini ni yule anayetazama mambo yaliyo muhimu na kuyazingatia, si vizuri kusikiliza sana yale yanayokuwa yakisemwa juu yako unapokuwa mchezaji.

Unapocheza vizuri watu wakakusifia inamfanya mchezaji ajisikie
vizuri, lakini ukisemwa vibaya unatakiwa kuwa na umakini wa ziada ili kutofanya makosa zaidi. 
Nadir, amecheza na walinzi wengi wa kati katika klabu yake tangu aliposajiliwa mwaka 2007. Lulanga Mapunda, Wisdom Ndlovu,Isack Boakey, Chacha Marwa, Ibrahimu Job, Mbuyu Twite,
ila kiwango chake cha sasa akicheza na Kelvin kinaonesha kuimarika na kupevuka kiuchezaji. Ni wakati mzuri sasa kwa upande wake, na timu yake pia.

Nadir, ametokea kujiamini sana, kupunguza papara, kuondosha mipira inayoingia katika maeneo yao ya hatari, amekuwa akiwapanga wenzake na yeye binafsi katika mchezo, jambo ambalo limemfanya kucheza akiwa huru na kujiamini. 
Kama watazidi kuboresha mahusiano yao ya kiuchezaji na
Kelvin, Nadir atacheza kwa muda mrefu katika timu hiyo kawaida.
Lakini ni lazima kufanya jitihada kuzuia hilo kadri iwezekanavyo.
Mlinzi makini ni yule anayetazama mambo yaliyo muhimu na kuyazingatia

Si vizuri kusikiliza sana yale yanayokuwa yakisemwa juu yako unapokuwa mchezaji. Unapocheza vizuri watu wakakusifia inamfanya mchezaji ajisikie vizuri, lakini ukisemwa vibaya unatakiwa kuwa na umakini wa ziada ili kutofanya makosa zaidi. 

Nadir, amecheza na walinzi wengi wa kati katika klabu yake tangu aliposajiliwa mwaka 2007. 
Lulanga Mapunda, Wisdom Ndlovu,Isack Boakey, Chacha Marwa, Ibrahimu Job, Mbuyu Twite, ila kiwango chake cha sasa akicheza na Kelvin kinaonesha kuimarika na kupevuka kiuchezaji. Ni wakati mzuri sasa kwa upande wake, na timu yake pia. Ukuta wa Yanga umeimarika sasa, na kiwango cha Nadir kinapelekea safu nzima ya ulinzi kucheza kwa mpangilio na umakini wa kuepuka makosa yasiyo na ulazima.