MSHAMBULIAJI
Lionel Messi amepiga hat-trick usiku huu Barcelona ikishinda 4-3 dhidi
ya Real Madrid katika mchezo wa La Liga uliofanyika Uwanja wa Santiago
Bernabeu mjini Madrid.
Andres
Iniesta alianza kuifungia Barcelona dakika ya saba, Karim Benzema
akaisawazishia Real dakika ya 20 na kufunga la pili dakika ya 24.
Barcelona
ikazinduka na kupata bao la kusawazisha dakika ya 42 kupitia kwa Messi,
lakini Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo akaifungia Real bao
la tatu dakika ya 55 kwa penalti.


Sergio Ramos akishangilia bao la tatu la Madrid na Ronaldo (kushoto) wakati nyota huyo wa Madrid anaonekana akiruka kulia
Messi
akafunga mara mbili mfululizo kwa penalti dakika za 65 na 84
kukamilisha hat trick yake Barcelona ikifufua matumaini ya kutetea
ubingwa wake msimu huu.
Real
Ilimpoteza beki wake Sergio Ramos aliyetolewa nje kwa kadi nyekundu
dakika ya 63 kwa kumuangusha Neymar kwenye eneo la hatari, wakati Pepe,
Di Maria, Alonso, Modric na Ronaldo wote walionyeshwa kadi za njano na
kwa upande wa Barcelona, Fabregas na Busquets pia walionywa kwa kadi za
njano.
Kwa
matokeo hayo Real inabaki na pointi zake 70, ingawa inaendelea kuongoza
La Liga kwa wastani wa mabao, ikiwa inalingana pointi na Atletico
Madrid, ambayo mapema iliifunga Real Betis 2-0, mabao ya Gabi dakika ya
58 na Diego Costa 64, wakati Barcelona inabaki nafasi ya tatu licha ya
kufikisha pointi 69. Barca na Real zimecheza mechi 28 kila moja, wakati
Atletico imecheza mechi moja zaidi.
Kikosi
cha Real Madrid kilikuwa: Diego Lopez, Pepe, Ramos, Cristiano Ronaldo,
Benzema/Varane dk64, Bale, Marcelo, Xabi Alonso, Carvajal, Modric/Morata
dk90 na Di Maria/Isco dk85.
Barcelona:
Valdes, Alves, Piqué, Mascherano, Jordi Alba, Sergio, Xavi, Iniesta,
Fabregas/Sanchez, dk78, Messi na Neymar/Pedro dk69.

Lionel Messi akifunga katikati ya msitu wa wachezaji wa Real

Javier Mascherano na kipa Victor Valdes wakiwa chini, huku Benzema akitimka kushangilia baada ya kufunga

Karim Benzema amefunga mabao mawili

Benzema akigombea mpira wa juu na Mascherano

Neymar akiwatazama Pepe na Fabregas wakifanyiana ubabe

Fabregas na Pepe wote waliishia kuanguka na wote wakaonyeshwa kadi za njano

Bale akipambana na Iniesta

Cristiano Ronaldo akilalamika baada ya kuchezewa rafu

Mashabiki wawili wa Real Madrid wakiwa na bango la kumtukuza Cristiano Ronaldo "Ameumbwa peponi".

