Friday, 21 March 2014

Loga aja na mfumo wa Bundesliga Simba

Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic.

Na Nicodemus Jonas
KOCHA Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amesema ameamua kuanzisha mfumo mpya wa kupiga mashuti na ameanza kuwafundisha tangu Jumatatu ya wiki hii.
Mfumo huu wa kupiga mashuti nje ya eneo la 18 ni maarufu katika Ligi ya Kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’, ambapo Loga amesema ameamua kuufanyia kazi kutokana na wachezaji wake ‘kutojiongeza’ badala yake wanakalia kupiga pasi pekee.

Aliongeza kuwa, hakuna straika ambaye wake ambaye amekuwa na tabia ya kupiga mashuti mkali langoni kitu ambacho hakimfurahishi.
“Wachezaji wangu wanakosa maamuzi binafsi ambayo yanaweza kuwa tija kwa timu. Hakuna straika wala kiungo ambaye anajaribu shuti langoni, badala yake wapo bize na kupiga pasi wakilazimisha kuingia ndani ya box.
“Siyo vibaya, lakini kuna wakati tunakuwa na nafasi ya mashuti lakini hakuna mtu mwenye akili ya maamuzi hayo, ndiyo maana nimeamua kulifanyia kazi tangu Jumatatu