Kutokana
na mgomo huo ndipo madereva wa magari hayo na makondakta wakaamua
kugeuza stendi hiyo uwanja wa mpira wa miguu likapigwa mbungi kati ya
madereva na makondakta.
|
Ndipo askari walipoamua kuingilia kati na kuzuia mchezo huo uliokuwa hauna waamuzi wala milingoti ya kufunga magoli.
|
Baadhi ya makondakta na madereva wa magari hayo wakatiwa mikononi.
|
Hata
hivyo hatua ya kukamatwa kwa madereva na makundakta kiliwatia hasira
wapiga debe wakaamua kulipopoa gari la polisi kwa mawe na kuvunja kioo
cha nyuma kama inavyoonekana hapa.
|
Abiria walilazimika kupanda gari la kusafirisha magazeti.Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii ,Moshi
|