Jeshi la
polisi wilayani Nzega mkoani Tabora limetumia nguvu kusambaratisha
maandamano ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu yaliyolenga kupinga kufungwa kwa machimbo yao ya Mwashina yaliyo jirani na mgodi wa Resolute Tanzania Limited wilayani Nzega.
Mara
baada ya kukaribia katika eneo la machimbo ambako maandamano yalikuwa
yanaelekea,kabla hata hawajafika eneo la machimbo,ghafla polisi
waliibuka na kuanza kurusha mabomu hovyo na baadaye kumkata mbunge wa
jimbo la Nzega Dkt Hamis Kigwangalla ambaye kabla ya kuanza kwa
maandamano hayo alifanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nzega
ndogo ili kujua mstakabali wa wachimbaji hao ambao hivi karibuni
waliziuiwa kuchumba na kamishana wa madini nchini Paul Masanja kwa kile
kilichotajwa kuwa wamevamia eneo hilo.
Kufuatia
malalamiko ya wachimbaji hao kuondolewa bila kujali gharama
waliozotumia walimwomba mbunge wao aridhie maandamano hadi katika eneo
la machimbo ndipo mkutano ukavunjika na maandamano yakaanza na matokeo
yake mabomu ya machozi pamoja na risasi za moto.
Katika na
purukushani hizo polisi walifanikiwa kumkamata mbunge huyo na kumjeruhi
mtu mmoja kwa risasi ya moto kwenye paji la uso ambapo waliondoka nae
kwenye gari pamoja na mbunge huyo.
Katika
hatua nyingine hali ilikuwa tete kwa waandishi wa habari kwani askari
wa jeshi hilo waliziba njia na kuwazuia waandishi wa habari kufanya kazi
zao kwa vitisho mbalimbali na matumisi ingawa hali hiyo ilitulia baada
ya maandamano ya wachimbaji kujitokeza.